Ni rahisi kwa Mzazi wa Kiafrika kukutukana kuliko kukwambia 'Nakupenda Mwanangu'

Ni rahisi kwa Mzazi wa Kiafrika kukutukana kuliko kukwambia 'Nakupenda Mwanangu'

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1687080660787.png

Malezi ya Kiafrika yana changamoto sana, licha ya kuwa kila mzazi ana njia zake za kumlea mtoto lakini kwa Afrika huku nyingi zinafanana, ikiwemo kuchapa, kufokea, kutukana, kusemwa vibaya na mengine mengi. Hali imesababisha madhara makubwa kwa watoto wengi na kuharibu tabia kiasi cha kuwa wazazi wenye matendo kama waliyolelewa wao.

Huku familia nyingi ni nadra kumuona Baba anamwambia Mama 'Nakupenda Mke Wangu' au hata kumbusu tu mbele ya Watoto. Jambo hilo limefanya watoto wengi kuishi wakiamini kuonesha upendo hadharani ni jambo baya. Wengine mpaka wamekuwa watu wazima hawajawahi kutamkiwa neno 'NAKUPENDA' kutoka kwa mzazi.

Wazazi wa Kiafrika wanafikiria kumpa mtoto fedha au kumtunza kwa kumpa mahitaji yake pekee ndio UPENDO, wakati ule ni Wajibu wa mzazi kwa mtoto. Ndugu mzazi unatakiwa kuwajibika kwa Mwanao Kihisia zaidi kuliko hata kifedha. Malezi ya kumjenga mtoto wako kimaadili na kwa kauli zako ni bora zaidi kuliko kumpa hela kila anapohitaji.

Ndio maana ukiangalia familia nyingi za kitajiri huwa zinatoa watoto wenye tabia za hovyo sana kwasababu wazazo wanakuwa available kiuchumi zaidi kuliko kihisia.
 
Matendo mengi sana ya Mzazi wa ki Africa yanawakilisha Upendo, hata kama hasemi.

UZUNGU mnaouona kwenye tamthiliya, mnadanganyana nao tu, hakuna watu wa hovyo kama hao.

Wazazi walipe ada, wakupe chakula, wakupe mavazi na maitaji, Huo ndo Upendo, hata kama hawasemi.
 
Kwani hao wazungu watoto wao hujihudumia pamoja na kujilipia ada?

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Matendo mengi sana ya Mzazi wa ki Africa yanawakilisha Upendo, hata kama hasemi.

UZUNGU mnaouona kwenye tamthiliya, mnadanganyana nao tu, hakuna watu wa hovyo kama hao.

Wazazi walipe ada, wakupe chakula, wakupe mavazi na maitaji, Huo ndo Upendo, hata kama hawasemi.
Kabisaa mkuu.Mzaz wa kiafrika ndio mfano wa malezi bora for the whole human kind
 
Hii mada uaipotajwa Ushoga hapa, huu uzi ni batili.
Nipo na [emoji897]nimekaa palee.
 
Matendo mengi sana ya Mzazi wa ki Africa yanawakilisha Upendo, hata kama hasemi.

UZUNGU mnaouona kwenye tamthiliya, mnadanganyana nao tu, hakuna watu wa hovyo kama hao.

Wazazi walipe ada, wakupe chakula, wakupe mavazi na maitaji, Huo ndo Upendo, hata kama hawasemi.
Huo ni wajibu sio upendo. Hata kama humpendi mwanao huwezi muua kwa njaa lazima umpe chakula.
 
Huo ni wajibu sio upendo. Hata kama humpendi mwanao huwezi muua kwa njaa lazima umpe chakula.
NI kwel kuna wajibu halaf kuna upendo .Ni vitu viwil tofauti LAKINI ukiona mtu anatimiza wajibu wake fully, jua kabisa ni UPENDO ndani yake UNAMSUKUMA kufanya hayo yote.
Ndio maana unaona wapo wenye uwezo wao wa kutimiza wajibu lakin hawafanyi hivyo japo ni watoto wao wa kuwazaa na kuna wale wazaz hawana kitu ila wanafanya juu chini watoto wao wasikose kitu kabisaa.

Swali!.

WEWE NI MZAZI???
kama ni mzazi basi utaelewa kile nasema
 
Ila miaka ya karibuni watu wameanza kubadilika mkuu.

Kwa sasa watoto wana confidence sana, kuuliza asipoelewa anauliza.
Tofauti na zamani mzazi unamuogopa kama simba vile, huwezi kuhoji, hashauriki, huwezi sema baba napenda kile au hiki, atakachosema yeye ndio hichohicho.
 
Endeleeni kupuuza utamaduni wenu, huo ndo utambulisho wenu.
Hakuna anayepuuza utamaduni, ila kuna mengine lazima yaachwe, hiki tuu kifaa tunachotumia wewe na mie wametengeza hao hao tunawagawia malighafi kisha wanatuletea simu, sie kukenua tu.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom