BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Malezi ya Kiafrika yana changamoto sana, licha ya kuwa kila mzazi ana njia zake za kumlea mtoto lakini kwa Afrika huku nyingi zinafanana, ikiwemo kuchapa, kufokea, kutukana, kusemwa vibaya na mengine mengi. Hali imesababisha madhara makubwa kwa watoto wengi na kuharibu tabia kiasi cha kuwa wazazi wenye matendo kama waliyolelewa wao.
Huku familia nyingi ni nadra kumuona Baba anamwambia Mama 'Nakupenda Mke Wangu' au hata kumbusu tu mbele ya Watoto. Jambo hilo limefanya watoto wengi kuishi wakiamini kuonesha upendo hadharani ni jambo baya. Wengine mpaka wamekuwa watu wazima hawajawahi kutamkiwa neno 'NAKUPENDA' kutoka kwa mzazi.
Wazazi wa Kiafrika wanafikiria kumpa mtoto fedha au kumtunza kwa kumpa mahitaji yake pekee ndio UPENDO, wakati ule ni Wajibu wa mzazi kwa mtoto. Ndugu mzazi unatakiwa kuwajibika kwa Mwanao Kihisia zaidi kuliko hata kifedha. Malezi ya kumjenga mtoto wako kimaadili na kwa kauli zako ni bora zaidi kuliko kumpa hela kila anapohitaji.
Ndio maana ukiangalia familia nyingi za kitajiri huwa zinatoa watoto wenye tabia za hovyo sana kwasababu wazazo wanakuwa available kiuchumi zaidi kuliko kihisia.