Ni rasmi sasa 2025 ni Samia vs Lissu?

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Baada ya Rais Samia leo kuweka bayana kuwa atajitosa kuwania urais mwaka 2025 ni dhahiri sasa mpambano wa kuwania kiti hicho utakuwa kati yake na makamu mwenyekiti wa Chadema aliyekimbilia Ubelgiji Tundu Lissu.

Kuanzia sasa wananchi wataanza kuwachekecha kwenye chujio kali la nani anafaa zaidi muda utakapofika.
 
Lisu hata akipambanishwa na Pole pole ataangukia pua tu. Jamaa ameshindwa kuwashawishi watanzania wakipatie chama chake hata wabunge watano, sembuse uraisi!
 
2025 wapinzani wanatakiwa kuunda chama kipya

Kisiwe chadema, cuf, Act, wala chochote

Wapinzani tunatakiwa tuje kivingine

Tufanane fanane na kule south kwa julias malema au uganda kwa bobi wine

Wapinzani tuunde chama cha vijana

Tuje pamoja kama vijana wa upinzani kutoka vyama vyote vya siasa vyenye baraza la vijana

Mbowe, zito, lisu, lema, msigwa, sugu, lipumba nk

Wote hao zilipendwa awana tena mvuto

Kama tukija na mkakati huo 2925 CCM hii ya samia chaliii

Lakini tukileta tena ubinafsi wa chadema, Act, cuf

Hakuna mpinzani ataweza kuiangusha CCM kwa sura za hawa wakina lisu,mbowe,lipumba,zito,lema wananchi sio wajinga wataona ni kheri zimwi likujualo kuliko hao wapinzani wachumia Tumbo
 
Karne 9 zijazo
 
Nakubaliana na wewe mkuu. CCM kutoka madarakani ni 2925
 
Tusipotezeane muda kujadili kitu ambacho kipo wazi
Wanaongoza nchi wapo pembeni wala awana shida tena ya kubadirisha mtawala
huyu mama yupo pale mpaka 2025 /2030
Sisi kama wapinzani ndio tunatakiwa kujipanga
Ccm wao wameshamaliza kazi
Anayepewa kijiti ni mpaka amalize miaka yake 10
Mama anatawala kwa rimoti kutoka timu msoga hakuna wa kumtoa pale....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…