Ni rasmi sasa nimeingia kwenye penzi na binti wa duka langu, nichukue tahadhari zipi ili kuepuka shari kamili

Siku kikinuka uje ulete mrejeshon tena. Kuna Bwashemeji wangu kafanya ujinga wa design hiyo hiyo copy na kupaste. Leo hii hana pa kushika tena. Amemuoa dada yangu. wakafungua duka jamaa akaamua kutembea na dada wa dukani. kilichofuata mahesabu dukani yakawa yanavurugika tuu. Kibaya zaidi akaamua kufanya wazi hadi mkewe akajua, na haikuishia hapo akazaa naye akampangia chumba kabisa kama mke wa pili. Ndoa yao iliparanganyika hadi sasa hakieleweki. Dadangu ni muajiriwa na ana mshahara mzuri tuu. akaamua kujitoa kwenye biashara za mumewe zote. sasa hivi jamaa anazidi tu kuzaa na mabinti wengine. huyu mke wa pili ambaye alikuwa muuza duka naye ashatelekezwa kwa maana kila siku wanazaliwa warembo wapya tuu.
 
Nimeanzisha kanisa mtoa mada utakua msoma neno
 
Mtoto ni mgeni hapa duniani (Mch. Hananja, 2023). Binti wa miaka 19 unamuita mchepuko? So sad. Binti mdogo anaharibiwa future hivihivi. Siku huyo binti ukija kumuacha bahati nzuri asiwe na mtoto wala mimba atakua amejaa sumu juu ya wanaume. Ukimwacha na mtoto ndio kabisaa haijalishi utahudumia au la.

Ndio maana siku hizi unamkuta binti mdogo hana hisia na wanaume kabisa. Kumbe binti wawatu alishapigwa matukio na wapuuzi kama nyie hadi ameiva.

Anyway, all the best buddy
 
biashara na ngono huwa haviendi sambamba hata kidogo RIp duka
 
Bora amwache achezewe na bachelor sio walio ndoani ambao ni moja kwa zote uwezekano wa kuolewa nao ni 0.00.

Jamaa kafeli sana kiukweli
 
[emoji419][emoji419]nakazia
 
Kiukweli hivi vitu vinaumiza sana ni vile MTU unakosa namna ya kutoa msaada.
 
Miaka 28 kwa 19 how comes? Hii ni ukatili wa kiutu. Ubinafsi ni kwa aliyezaa nae. Hapo kwa huyu mwengine ni torturing.
 
Jiandae hilo duka kufunguliwa na kufungwa muda wowote, [emoji23][emoji23][emoji23] mvua ikinyesha tu anaumwa, mahesabu tena ndiyo basi
 
Kumbuka dhambi ya zinaa ni deni unachokifanya kwa bint wa watu tena uku ukijisifia kabisa huna mpango nae...elewa kwamba na ww utazaa mtoto wa kike akija kulipa deni lako usije ukatafuta mchawi ukumbuke matukio yako ya haya machafu unayojigamvmba nayo leo kwa kitoto cha watu.....siwezi kumlaumu huyo mtoto kwakua ww ndio umemuanza na tayari kama bint amekua na matarajio ya starah na kadhalika na huwenda yeye anakuchukulia kwa mtazamo mzuri tu lkn kumbe ww ni fisi
 
Binadamu mmekua ni wanyama sana utu umepotea kabisa ndio mana dunia imekua sehemu ya shida na mabalaa....yaani unawaza kuharibikiwa biashara yako na wala huwazi kwamba unamuharibia feauture mtoto wa watu kwakua yeye anamatarajio na ww unamuona kama toi ambalo halina maana ...siku akigundua ushenzi wako juu yake chozi likimotoka kwa ulivyompotezea muda namkulaghai unafikiri wewe utakua salama
 
Yaani unashauriwa halafu unapuuza, unakuja tena kuomba ushauri, dogo unatuchuliaje wanajf,??
Huyu tayari ana plan zake, hapa anakuja kutusimulia tu. Yani anatengeneza hadi uzi wa kushukuru ushauri kua katuliza tamaa, alafu analeta mwingine tumshauri namna ya kuzitendea kazi tamaa zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…