Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimestushwa Sana na taarifa iliyotolewa Ikulu, ikionyesha kuwa wakuu wa wilaya 48, wamehamishwa vituo vyao vya kazi.
Hivi Rais anawezaje kuwahamisha wakuu wa wilaya 48, Ili waende kwenye vituo vyao vipya vya kazi?
Pia nimuulize Rais, je alipokuwa anafanya uteuzi huo, hakujua mapungufu ya wakuu hao wa wilaya?
Kwa kuwa Mimi kama raia wa nchi hii, nina wajibu wa kuliuliza hili, Kwa kuwa najua uhamisho wowote, hususani wa hao vigogo, unaligharimu Taifa hili mabilioni ya pesa za uhamisho, ambazo tutakamuliwa Kwa Kodi na tozo Mimi na Wewe!
Hivi kama mamlaka ya uteuzi limegundua kuwa hao wakuu wa wilaya walifanya "madudu" kwenye vituo vyao vya awali, ni kwanini wasipigwe chini na kuachishwa kazi badala ya kuwahamisha vituo vyao vya kazi, ambapo mzigo wa kuwalipia hiyo inayoitwa "transfer allowance" tunaibeba sisi walipa Kodi wa nchi hii?
Hivi katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapitia kipindi kigumu mno, Cha upandaji wa gharama za maisha, hususani bei vya vyakula, ndiyo Serikali yetu, inatumia matumizi mabaya kiasi hicho Cha kuwalipia mabilioni ya pesa, wateule hao wa Rais?
Ndio maana tunaungana na hoja kuu ya Chama kikuu Cha upinzani nchini Cha Chadema, kuwa Taifa hili Kwa hivi Sasa linahitaji kuwa na Katiba mpya ambayo itampunguzia Kwa kiasi kikubwa madaraka makubwa mno aliyo nayo Rais wetu.
Ikumbukwe kuwa yeye Rais ndiye anayewateua wakuu wote wa wilaya 140 nchini na Wala huwezi muuliza, ni vigezo gani alivyotumia, katika uteuzi wake!
Pia ndiye anayewateua wakurugenzi wa wilaya, Kwa idadi hiyo hiyo ya 140
Pia ndiye anayewateua Mkuu wa Jeshi, IGP,Mkurugenzi wa Uchaguzi, Majaji na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali za mashirika ya Umma
Haya madaraka makubwa mno ya ki-mungu-mtu ambayo Rais wa Taifa letu, amepewa na Katiba ya nchi yetu, ndiyo inayoliangamiza Taifa letu!