Ni sahihi kijana wa karne hii kufuata ushauri wa "wazee" katika ndoa au mahusiano?

Ni sahihi kijana wa karne hii kufuata ushauri wa "wazee" katika ndoa au mahusiano?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nyakati zimebadilika sana, wanawake single mothers , talaka kwa Wakristo na ndoa kwa watu wa makabila tofauti sio mwiko(taboo) tena, katika mazingira haya je kuna haja ya kuwasikiliza na kuwatilia maanani wazee walioishi karne hiyo kuhusiana na masuala ya ndoa au mahusiano?

Screenshot_20240816-104642_X.jpg
 
Hivi Pesa inavyotuvuruga, unaweza pata Mchumba wa kike masikini,
kisha mzazi wa mwanaume akamshauli mwanae usiowe mtoto wa kimaskini hivo unaongeza mizigo kwenye ukoo wetu.

Haya maisha saivi ni kujisimamia tu kimaamuzi, liwalo na liwe ili yatakayokuja kutokea usilaumu mtu.
 
Inawezekana ukawa sio sahihi kwa sababu zamani ndio kulikuwa na ndoa . Maisha ya sasa ndio sio applicable sana kutokana na kukosa misingi halisi ya ndoa , kuoa sio lazima ila ni muhimu .

Ukioa single mother , mwajiriwa, aliyeyelewa na mzazi mmoja , kiburi , mwizi, mpenda starehe , hawa wa vikuku, wale wa vigodoro na miziki , na wengine wengi wote ni matatizo hamna ndoa hapo .
 
Uko serious?
 
Binadamu ni kiumbe complex mno hivyo hakuna sheria na mwongozo jumuishi juu yake. Ni lazima umtazame mtu mmojammoja badala ya kumjumuisha katika kundi.

Wapo waliolelewa na wazazi wote na ni wa ovyo, wapo waliolelewa na mzazi mmoja ni wa maana na tupo sisi ambao muda mwingi kwenye makuzi yetu hatujalelewa na mzazi mmojawapo na tumenyooka.
 
Wazee wenyewe hawakubaliani.

Mfano kuna wazee watakuambia usioe kabila fulani, wengine watakuambia makabila hayana shida, shida ni dini.

Unafanya tu unachokiona ni sawa, ukikosea pakubwa kuna ile crowd psychology, utajikuta unakosolewa na watu wengi....
 
USHAURI haukuamulii, ila unakupa MACHAGUZI mengine.

mfano mie nina milioni 10, nataka ninunue kiwanja akili imegota huko, mwingine atakuja kuniambia nunua gari, mwingine anzisha biashara fulanj, mwingine biashara hii, mwingine tuweke heshima bar, tumia pesa ikuzoee mzee..

Hawa hawanichagulii, ila ushauri wao unaniongezea uchaguzi wa maamuzi, nikichanganya za kuambiwa na za kwangu huenda nikapata kilicho bora zaidi, naweza pia nikapiga ushauri wao chini na kuendelea na uamuzi wangu.
 
Back
Top Bottom