Ni sahihi kuchimba kisima maji kipindi cha masika?

Futi 250 !!!? Hiyo hapana, chukulia futi 40 ni sawa na mlingoti wa umeme au container lile kubwa .

Sasa pima kwenda chini, kwa jinsi walivyochimba kwangu na uzoefu nilioupata uwezekano wa kawaida kuchimba bila kuhitaji nyongeza ya HEWA ni futi 80.
Kwa mujibu wa maelezo yake, anaweza kuchimba hata zaidi ya futi 150 kwenda chini, lakini mimi sikihitaji kirefu kiasi hicho. Naamini maji yapo umbali usiozidi futi 30 chini ya ardhi.
 
1. Ndio uwezekano wa kisima kilichochimbwa kwa mikono wakati wa masika ni mkubwa sana, kwa sababu wakati kina cha maji ya ardhini hupanda wakati wa masika hivyo maji kuapatikana na katika kina kifupi, na hushuka katika kipindi cha kiangazi hivyo maji hupatikana katika kina kirefu.

Haisumbui kuchimba kisima muda wa kiangazi au masika, ila kinachotakikana ni kwa mchimbaji kuwa na uelewa wa haidrojiolojia ya eneo husika, na hapa ndipo unakuja umuhimu wa mchimbaji kufanya kautafiti ili kufanya maamuzi sahihi ya urefu wa kisima.
 
2. Kuhusu kuongeza urefu wa kisima baada ya kukichimba, hiyo inategemea na namna kisima kilivyochimbwa na kudizainiwa.
 
Hivi kuna sehemu hata wakitoboa futi nyingi kwenda chini hawakuti maji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…