Ni sahihi kujinunulia majeneza na kujijengea kaburi?

Ni sahihi kujinunulia majeneza na kujijengea kaburi?

Angalia huyu hapa Equation x alichofanya 👇🏿.
Sijui ni kitu gani kilichomsukuma kufanya hivyo?
 
Inahitaji ujasiri kufanya hivyo?
Mkuu kama umejiandaa vya kutosha, familia ipo njema na Ac. Inasoma na unaona ushazeeka au unaumwaumwa na la MSINGI unauhakika na unapoenda baada ya kufa.

Andaa hadi suti, marumaru na edit kabisa maandishi yatakayosomeka juu ya kaburi lako kwa kuchagua maandiko uyapendayo na yakisindikizwa na m/mistari matata na kuchagua picha matata ya kukumbukwa kwayo.



Kwa mimi ningeweka mstari huu[emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313]

Ufu 14:13 SUV

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Itazoeleka na kuonekana kawaida sana. Miaka ya nyuma late 80's and early 90's majeneza yalipoanza kuchongwa kusubiri wateja badala ya fundi kutafutwa baada ya tukio ilionekana kitu cha ajabu mno!

Leo hii majeneza yamezagaa kila mtaa na yamekuwa msaada mkubwa na bidhaa muhimu kwa maisha. Leo bodaboda, guta, etc. zinabeba caskets and no one cares unapokutana nayo.

Hata gari special za maiti zilipoanza kuingia ilionekana so unusual ila leo unaweka order mapema kupata huduma. Muda ni Mwalimu mzuri.
 
Kwa upande wangu si sahihi..kila mtu afanye atakacho as long as si kinyume Cha sheria ya nchi.
 
Me nataka nikifa nisizikwe ,viungo vyangu vitumiwe kwenye majaribio ya kisayansi !! Baadhi ya viungo wavidonate kwa wanaohitaji , lile skeleton kama litabaki baada ya majaribio lipambwe !!
 
Kama si kosa kisheria na kijamii sio tatizo, itasaidia kubebesha watu gharama za mazishi, ikiwezekana waweke na bank pesa kabisa za kugharamia maziko.
kuna vipimo vya mwili wa upcoming maiti vinachukuliwa???

Na je what if kama marehem atavimba(maana kuna baadhi ya vyanzo vya kifo vinasababisha mwili kuvimba)

Je hiyo budget anayosema kwamba asisumbue watu inahusisha pia na ela ya uber??

Je kuna watu hatuli nyama ya miguu minne km vile ngombe,mbuzi
Tushazoea kuku,bata n.k labda kidoooogooooo fire chair!!! Hiyo budget inakuwepo?
 
Hii dhana ya kujinunulia majenezo au kujijengea makaburi kabla ya kifo chako, kwa kisingizio eti ukifa usije kusumbua watu katika michango.

Hii imekaaje wakuu? Ni sawa kufanya hivyo?
Mila na destruri zetu , haiko sawa. Ni mambo ya kuiga destruri za watu wengine.
 
Siku hizi hata BIMA ya maisha ipo tu, ni wewe kuamua kujilipia BIMA yako na familia yako endapo kifo kikikupata.

Mfano CRDB bank kupitia ALLIANCE wana BIMA ya maisha, unachangia 48,000 kwa mwaka unakuwa guaranteed wewe na familia yako mwaka mzima, likitokea jambo they take care of the costs... around 10,000,000 akifa mume, 5,000,000 akifa mke na watoto 3,000,000.

Mambo yanaenda kasi sana duniani.
 
Back
Top Bottom