Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Umepotosha
 
Kuna siku jamaa alikuja home ndo tuko mezani tunapata msosi na kulikuwa na kuku. Mimi nikamkaribisha mwana na nikampakulia kabisa na vipande vya kuku, alishukuru tu ila alikula mboga za majani hakugusa kabisa ile nyama ya kuku. Sikumuona wakati akila so sikujua kama hakula badae naangalia mezani nakuta ile mboga iko vilevile ilibidi nimuulize vipihutumii kuku siku hii ndo akanishtua suala la kuchinja aisee nilistaajabu
 
Hapana Muislam haruhusiwi kula nyama ya mzoga au aliechinjwa kwa jina lisilokua la Mwenyezi Mungu.
Hivi mkifika mahotelini huwa mnauliza aliyechinja ni wa dini ipi?
 
Waislam ni watu wa ajabu sana,wenyewe hawataki kula nyama iliyochinjwa na Mkristo,sasa sijui wanadhani wakristo ndio wanapenda kula mnyama aliye chinjwa na Muslims?
Wapi imekatazwa nionyeshe kweny maandiko? Mzogo na kibudu ni haramu
 
Nyama ambayo imechinjwa kwa njia sahihi haina tatizo , ila kuna ile mifumo kama wanavyochinja nguruwe wanamuua kwanza kwa magongo halafu ndio anachinjwa kifupi ni kibudu 😀 .

Kunyanyasa wanyama kwa kuwaua kwanza ndio uchinje yaani washakufa hata damu haitembei, wale kuku wa sigida wengi wanakuwa wamekufa yaani kibudu halafu ndio wanachinjwa hii haifai kwa mtu wa dini yoyote ile.
 
Hata wewe huwezi kula mzogo au kibudu acha kuleta mjadala , ishu ipo wazi hata kisayansi ,
Jibu swali kwanza, mkienda hotelini kabla ya kuletewa MENU huwa mnauliza kwanza Mchinjaji ni wa dini ipi?
 
Jibu swali kwanza, mkienda hotelini kabla ya kuletewa MENU huwa mnauliza kwanza Mchinjaji ni wa dini ipi?
Nakuuliza wewe kibudu na mzogo ni halali kula? Hata wale hadzabe wanajua huu mzogo ni wa fisi na hiki ni kibudu
 
Kibudu ni nini? Naomba tuanzie hapo
kibudu ni mnyama aliyekufa ..Hakuna dini inayoruhusu kula kibudu wala wanyamapori labda Fisi tu.


Nyamafu ni nyama ya mnyama aliyekufa (kibudu) bila kuuliwa kwa asili (yaani kuchinjwa). Mungu aliwakataza wana wa Israeli katika agano la kale wasile nyama ya mnyama yoyote aliyekufa bila kuchinjwa..

 
Machinjio yote ya kisasa wanyama hukatwa kichwa na mashine na waislamu wanakula vizuri tu
 
Je ukimpiga risasi mnyama pori kama Mbogo akafa ndio ukachinja hii nayo ni kibudu ?.......maana kumpata akiwa hai ndio umkate shingo sio rahisi.
Unatakiwa umuwahi kumchinja kabla hajafa, hata hivyo kama muwindaji ni muislamu na alipiga Bismillah kabla ya kumtandika risasi huyo mnyama basi ni Hali kumla
 
Kidini ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…