Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kuheshimu imani ya mtu, hasa katika nchi isiyo na dini, ni suala nyeti sana. Ndiyo maana Watanzania wengi wanapotaka kufanya sherehe, kama si Waislamu, huhakikisha kuwa mchinjaji wa nyama itakayotumika ni Muislamu.

Lakini itakuwaje ikiwa wewe si Muislamu na ukatembelewa ghafla na rafiki Muislamu wakati unamla kuku uliyemchinja mwenyewe?

1. Utamkaribisha kujumuika nawe pamoja na kuwa unajua ulichinja bila kuzingatia imani ya Kiislamu?

2. Utamjulisha ukweli kuwa ulimchinja wewe mwenyewe ili aamue mwenyewe?

3. Utamwambia asubirie umwandalie cha kwake?

Upi utakuwa uamuzi wa busara?
 
Mbona wanakula katika migahawa na mahoteli pasipo hata kukaribishwa sembuse kuambiwa imechinjwa na Mfuasi wa dini ipi

Kwani huwa wanauliza hata aliyechinja ni nani?

Na katika mabucha ya kisasa ambayo wanyama wanachinjwa kwa Mashine, pia hawali?
 
Kwa hapa Tanzania hawana mashaka kwa sababu utaratibu wa uchinjaji uko wazi.

Sijajua wanakabilianaje na hizo changamoto wakiwa kwenye Mataifa ya Kikristo!
 
Kuheshimu imani ya mtu, hasa katika nchi isiyo na dini, ni suala nyeti sana. Ndiyo maana Watanzania wengi wanapotaka kufanya sherehe, kama si Waislamu, huhakikisha kuwa mchinjaji wa nyama itakayotumika ni Muislamu.

Lakini itakuwaje ikiwa wewe si Muislamu na ukatembelewa ghafla na rafiki Muislamu wakati unamla kuku uliyemchinja mwenyewe?

1. Utamkaribisha kujumuika nawe pamoja na kuwa unajua ulichinja bila kuzingatia imani ya Kiislamu?

2. Utamjulisha ukweli kuwa ulimchinja wewe mwenyewe ili aamue mwenyewe?

3. Utamwambia asubirie umwandalie cha kwake?

Upi utakuwa uamuzi wa busara?
Muislam anaruhusiwa kula alichochinja asiyekuwa Muislam. Ila tu mchinjaji awe amechinja kweli. Wasio waislam wana tabia ya kuwapiga wanyama au kuku wanamtumbukiza kwenye maji moto anakufa kisha wanaanza kumkata kata. Muislam hali kibudu tu, kitu ambacho hakikuchinjwa. Kama umechinja vizuri kabisa yafaa kula.
 
Hata mimi sili kibudu ingawa si Muislamu.

Nashukuru kwa Elimu. Nishajiuliza hili swali mara nyingi, ingawa sijawahi kuwauliza marafiki zangu wa dini ya Kiislamu.
 
Kama vile Wakristo wanavyompiga marungu nguruwe kisha wanamchinja. Vile haifai.
Na pale hujachinja, kuchinja ni kuua kwa kukata shingo. Ukishampiga marungu akafa inakuwa unamkata kata tu. Hiyo haifai.
 
Kwani huwa wanamwua kwa kutumia rungu? Nafikiri wanaotumia rungu ni kwa ajili ya kuwafanya kuwa wapole ili wawakate shingo kirahisi.

Mimi nimeshuhudia mara moja nguruwe amichinjwa. Hawakutumia rungu. Alikatwa nyuma ya shingo kwa panga hadi kichwa kikatenganishwa na kiwiliwili.
 
Back
Top Bottom