Ni Sahihi kumnunulia dada, mama au mama mkwe nguo za ndani?

Ni Sahihi kumnunulia dada, mama au mama mkwe nguo za ndani?

Duh. Ni ngumu. Lakini mimi nilishashuhudia kwa macho yangu mdada wa miaka 30+ alimnunulia baba yake mzazi boxer ambae alikuwa kalazwa hospitalini.

Ipo hivi nilikuwa na muuguza nugu yangu katika hospitali moja ambayo ina vyumba vyenye vitanda viwiliviwili katika room. Sasa huyu manzi akamleta baba yake mzazi na katika maongezi alifika hana nguo za kubadili. Binti akamwambia baba ake pumzika ntaenda mjini kukuletea afu kesho wakati ndugu wengine wanakuja wataleta nguo zilizopo home. Alitoka na aliporudi alikuja na nguo full yaani t shirt vest suruali malapa na BOXER. Mpaka leo hua najiuliza yule dem alipata wapi ujasiri wa kununua boxer kwa mzee wake. Mzee wake nakumbuka aliniambia tuu hawa ndio mabinti zetu wa siku hizi. Alikuwa around 60+
 
Kuona nguo za Ndani za Baba Yako au Mama Yako Ikiwemo Brazia ni laana tosha kwako.Wazazi mnatakiwa kuhakikisha mnaanika nguo zenu za Siri Kwa Siri maana ni SAWA na kumpa laana mtoto wako anapoziona na kutambua hizi ni nguo za ndani za Baba au Mama.
 
Labda kwa mila za huko kwenu.
Hii ni Kibiblia kabisa hutakiwi kuuona utupu wa Baba Yako au Mama Yako na sio hao tu hata ndugu zako wa karibu.Hutakiwi kuona nguo zao za Ndani sababu Moja Kwa Moja unapoziona lazima tu upate taswira ya utupu wao ulivyo ndiyo maana tunasema ni laana kuona nguo za Ndani za Baba au Mama hata wakijitetea wanaanika kwenye Jua Ili waondoe uvundo kama itakuwa ni hadharani ambapo watoto wao wanaona basi tayari wanakuwa wamewalaani watoto wao.

Nakupa mfano mdogo mtoto kaona Brazia ya mama yake ya sponchi kaianua na kaishika kaona ni laini Moja Moja Kwa Moja yupo katika hatari ya kupiga punyeto.Laana tayari alafu kumbuka na Yale mawazo anayokuwa nayo pia ni laana.
 
Mambo ya Walawi 18:6.,7.,8.,9.,10.,11.,12.,13.,14.,15.,16.,17.,18.,19.,20.,21.,22.,23.,24.,25.,26.
6. Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. 7. Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8. Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9. Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. 10. Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. 11. Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. 12. Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. 13. Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. 14. Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. 15. Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. 16. Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. 17. Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. 18. Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai. 19. Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. 20. Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21. Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. 22. Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. 24. Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25. na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26. Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
 
Back
Top Bottom