Unakosea sana Cariha, kusema "yeye ana uhuru wa kujiamulia maisha yake na kujitafutia kipato", that's very wrong na mindset za namna hiyo ndani ya ndoa ni sumu kali.
Ndani ya ndoa hatujiamulii, hatufanyi maamuzi ya mtu mmoja, tunakaa, tunazungumza na kufanya maamuzi kifamilia, iwe biashara, ujenzi, kusomesha/kusoma, watoto nk. Kama upo single, unajiamulia maisha yako, ukiwa kwenye taasisi hii nyeti kabisa hujiamulii, unakuja na wazo, mnashirikishana na kuamua as a family.
Take this with you and make sure you build a strong institution.