Ni sahihi kumuajiri mwanamke uliyezaa naye kwenye biashara yako?

Ni sahihi kumuajiri mwanamke uliyezaa naye kwenye biashara yako?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Habari wakuu?

Nilikuwa na wazo la kufungua biashara ya nguo wilayani Kahama, na changamoto niliyonayo ni usimamizi, na mimi pia nipo mbali na huo ukanda.

Nikiangalia haraka haraka kwenye databesi yangu, anayeweza kukaa huko na kusimamia hiyo biashara ni mchepuko wangu niliyezaa naye mtoto.

Kwa upande wake atanufaika kwa mshahara labda na mauzo yakiwa juu; ila umiliki unakuwa ni wa kwangu.

Hofu niliyonayo; je hawezi kuja kunizurumu au kunitapeli huko mbeleni; akijua kabisa hii biashara siyo ya kwake, bali anampambania mwanamke mwenzake aliyepo kwenye ndoa?

Karibuni kwa ushauri
 
Inawezekana, ila ni risk sana...
Kwanza ni vigumu kumrudi mara kwa mara pale anapoenda wrong
Pili, kama anaakili mbovu itadumaa hyo project
Tatu mkianza kukorofishana tu, ndio mwisho wa biashara
 
Kama unampenda mwanao,
Na Unaona KABISA akili au uzoefu wa baishara uyo mwanamke anao .

Basi Wee mfungulie tu,

Maana kuombwa ombwa Ela kill mara na mtu mwnyw yuko mbali na wewe Kuna KERO zake nyingi Sana tu mkuu.
 
Kama huna kazi na hizo Hela bhasi kagawie ombaomba aisee ila Ukisema umpe mchepuko asimamie biashara ni biashara kichaaa yani utakuja kuliaaa vibaya sanaaa...!!
 
Inawezekana, ila ni risk sana...
Kwanza ni vigumu kumrudi mara kwa mara pale anapoenda wrong
Pili, kama anaakili mbovu itadumaa hyo project
Tatu mkianza kukorofishana tu, ndio mwisho wa biashara
Au nimuajiri na kijana mwingine, ambaye atakuwa anaripoti kwangu?
 
Akiwa mkarimu anaweza kufungua duka lake kupitia biashara yako na akakukabidhi duka lako. Akiwa jangili anafungua duka lake na wewe uta funga biashara kwa kupata hasara.
Kweli mkuu, ingawa malengo yangu kama ataweza kukaa mwaka na faida kuonekana, itakuwa vizuri zaidi akiwa na la kwake. Ingawa bi mkubwa hatojua kama nimemuajiri mpinzani wake.
 
Kama unampenda mwanao,
Na Unaona KABISA akili au uzoefu wa baishara uyo mwanamke anao .

Basi Wee mfungulie tu,

Maana kuombwa ombwa Ela kill mara na mtu mwnyw yuko mbali na wewe Kuna KERO zake nyingi Sana tu mkuu.
Nampenda sana mtoto; ila kwa sasa sitaki nyumbani wafahamu
 
Back
Top Bottom