Ni sahihi kumuajiri mwanamke uliyezaa naye kwenye biashara yako?

Ni sahihi kumuajiri mwanamke uliyezaa naye kwenye biashara yako?

Kama hutaki wafahamu Basi wazo la kumfungulia biashara litakusaidia kupunguza kupigiwa Simu za kila Mara mtoto kameza shoka.
inahitajika pesa HARAKA apelekwe hospitali.


Pamoja na hayo bado ataendelea kumpigia simu za usumbufu kumuomba hela za kusema mtoto anaumwa n.k

Atamwambia biashara haitoki na hadithi chungu nzima.

Tabu itakuwa palepale.
 
Kama una uhakika kuwa hataleta shida kwenye ndoa yako na biashara yako mfungulie, kama una wasiwasi naye tafuta mtu mwingine ilimradi unamtimizia Mtoto wako mahitaji yake.
Kwa ushauri nilioupata humu, naona ni bora kama hali itaruhusu, awe na duka lake tu.
 
Inavyoelekea mke halali anajua hii pesa ya mtaji, hapa ndipo tatizo lilipo. Kama jamaa angekua na hela yake ya siri angefungua duka na akawa anatembelea maeneo hayo kukagua biashara na familia ndogo.
Kweli mkuu, hapo ndipo shida ilipo
 
Mi nafikiri kwakua kuna mtoto, muweke wazi kabisa ni kwa ajili ya faida yenu na mtoto wenu, Hiyo itafanya asiwe na tamaa.
Inaweza kuwa hivyo, ila umiliki utakuwa unasoma jina langu; na hiyo biashara itakuwa inafahamika nyumbani. Hapo sijajua kama ataweza kuvumilia kama muajiriwa
 
Inaweza kuwa hivyo, ila umiliki utakuwa unasoma jina langu; na hiyo biashara itakuwa inafahamika nyumbani. Hapo sijajua kama ataweza kuvumilia kama muajiriwa
Ila ikifahamika hadi nyumbani jua itakuletea shida siku yyte. Pale mkeo atakapolazimika kutaka kufatilia mauzo au kuengage. Nakushauri kama unataka kumuweka isome jina lako lakin usiifamishe nyumbani.
 
Back
Top Bottom