Je, Hawa wananchi ambao ni mastar na ma celebrities ambao pia ni wafanya biashara Wana uelewa wowote wa protokali za Kiserikali.
Nimeshangaa Mfanyabiashara mkubwa kabisa mwanamke mwenye mafanikio mengi akiwa amejijengea umaarufu mkubwa kupitia biashara zake, akitoa kauli tata inayoelekea kama ni kumjibu Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye ni Raia namba tatu baada ya maelekezo mahususi ya kutakiwa kukamatwa kwa Niffer ambaye aliendesha zoezi la Michango Kwa maafa ya Kariakoo kinyume na Sheria ama bila kibali cha ofisi ya Waziri Mkuu inayosimamia majanga na dharura za aina hiyo.
Unaweza Kusoma ujumbe wa Niffer kupitia mtandao wake wa kijamii hapa chini