Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

Hakuna tofauti ya ukatoliki na uislam

Zote zinamilikiwa na nchi za nje

Katoliki inamilikiwa na Roma(Italia)
Uislam ubamilikiwa na arabia
 
Abadili tu akizinguliwa si anarud tu alipotoka
Sio rahisi kiasi hicho. Unakuta mambo yanakuja kubadilika mshazaa watoto watatu au wanne, kubadili dini ina maana ndoa hakuna tena,mwanamke kuondoka ndoani kuwaacha watoto wanalelewa na mama wa kambo sio jambo rahisi. Saa nyingine itabidi ufe na tai shingoni uvumilie ndoa ngumu kwa ajili ya watoto. Inakuwa ni mateso kwa maisha yako yaliyobakia.

Afikiri kabla hajaamua.
 
Funga ndoa kiserikali kila mtu abaki na imani yake. Watoto wakikua wachague imani yao
 
Naombeni ushauri,

Mimi ni msichana ambaye kwa muda sijawa na mtu nilitangaza hapa nimepata mtu nimempenda amenipenda ila sasa kazi ipo yeye ni muislamu.

Nanataka nibadilishe dini kwetu wana imani tosha walishakata niolewe na dini tofauti kwao juzi tumeenda hali ndio hiyo nimechoka kabisa.

Naombeni ushauri maana wakristo hawatamki ndoa ila nikipata waislamu wanadai ndoa fasta
hata miezi sita hafikii so niko njia panda hadi now.
Acha ujinga, dini nowdays ni kampuni za watu za kukusanyia fedha. Kama unaiman juu ya uwepo wa Mungu mmoja, shughuri imekwisha.
Amia tu kwenye uislamu, wasikubabaishe. Wakikususa, mimi nakuwa ndugu yako.
 
Uislam haumlazimishi mtu kusilimu. Na hutakiwi kusilimu ati tu uolewe au umuoe muislam. Unatakiwa usilimu pale tu unapohisi umeikubali dini ya kiislamu coz unaempenda atakufa au muta achana je utaweza kudumu katika dini ya uislam. Je mukiachana mmoja wenu akienda katika dini tofauti je watoto wenu wachukue upande gani. Uislamu umeweka mpangilio wa urithi kwa mke, mume, watoto, jamaa wa marehemu na wazazi wa marehemu. Sasa je watoto urithi huo utafuata utaratibu gan. Mi ushauri wa kusilimu ama kuto kusilimu unatakiwa uendane na ridhaa ya kidini na sio kimapenzi.
By the way I am muslim
 
Yesu ni njia na kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila.....angali kuna roho inakufuatilia,kama wazazi wamekukatalia wasilikilize wazazi.
Hakuna sababu ya kimantiki au Kisayansi kwa kusema ule ukweli, kwamba mtu fulani ni Mkristo au Muislam eti kwa sababu anaihusudu dini. Ukweli ulio dhahiri ni mmoja tu kuwa tunafuata dini kwa sababu wazazi wetu tuliwakuta wakiwa huko,nje ya hapo hakuna lolote. Na kwa sababu hiyo,tunafuata mkumbo. Huo ndiyo upande wa kwanza wa shillingi.
Ama kuhusu upande wa pili ni ule ambapo tayari tumo humo kwa kuzaliwa na kurithi dini,sasa suala linalofuata ni judgement based on belief and truth. Hilo inategemea na mapokea na tafakuri kuu,kupembua kwa undani uhalali wa kwa nini dini hii inasema hivi,ile inasema hivi. Ni suala la judgemental decision!
Uchaguzi unabaki kwa muhusika kupembua na kuamua dini ya haki ni ipi!
 
Naombeni ushauri,

Mimi ni msichana ambaye kwa muda sijawa na mtu nilitangaza hapa nimepata mtu nimempenda amenipenda ila sasa kazi ipo yeye ni muislamu.

Nanataka nibadilishe dini kwetu wana imani tosha walishakata niolewe na dini tofauti kwao juzi tumeenda hali ndio hiyo nimechoka kabisa.

Naombeni ushauri maana wakristo hawatamki ndoa ila nikipata waislamu wanadai ndoa fasta
hata miezi sita hafikii so niko njia panda hadi now.
Wanaotaka ndoa fasta pia niwaachaji/divorce wa haraka. Unasema "wakristo hawataki ndoa ila nikipata waislamu wanadai ndoa fasta" SWALI.:Kwani mwenzetu umeshaliwa na wangapi?
 
Wanaotaka ndoa fasta pia niwaachaji/divorce wa haraka. Unasema "wakristo hawataki ndoa ila nikipata waislamu wanadai ndoa fasta" SWALI.:Kwani mwenzetu umeshaliwa na wangapi?
😕😕😕😕 huu uzi upo kumbe???
 
Toka tu ukatoloki uingie uiskamu kwani lao moja , hakuna shehe mwanamke na mwanamke padri . Katofauti kadogo ni utatu mtakatifu ambao umetungwa kianaaina .
 
Dini zimetukuta..tulikuwa tunaabudu mawe enzi hizo....cha muhimu upendo tu
 
Hakuna sababu ya kimantiki au Kisayansi kwa kusema ule ukweli, kwamba mtu fulani ni Mkristo au Muislam eti kwa sababu anaihusudu dini. Ukweli ulio dhahiri ni mmoja tu kuwa tunafuata dini kwa sababu wazazi wetu tuliwakuta wakiwa huko,nje ya hapo hakuna lolote. Na kwa sababu hiyo,tunafuata mkumbo. Huo ndiyo upande wa kwanza wa shillingi.
Ama kuhusu upande wa pili ni ule ambapo tayari tumo humo kwa kuzaliwa na kurithi dini,sasa suala linalofuata ni judgement based on belief and truth. Hilo inategemea na mapokea na tafakuri kuu,kupembua kwa undani uhalali wa kwa nini dini hii inasema hivi,ile inasema hivi. Ni suala la judgemental decision!
Uchaguzi unabaki kwa muhusika kupembua na kuamua dini ya haki ni ipi!
Mkuu kuna watu wamezaliwa katika familia za kipagani, lakini wakisha kukua na kujitambua wanaingia dini wanayoichagua wenyewe, sasa hapo unasemaje eti wameridhi kwa wazazi? Kuna sababu nyingi. Lakini kubwa ni kuaminishwa kuhusu maisha ya kiroho ambayo ndiyo faraja ya maisha ya baadae.
 
Back
Top Bottom