Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

Naombeni ushauri,

Mimi ni msichana ambaye kwa muda sijawa na mtu nilitangaza hapa nimepata mtu nimempenda amenipenda ila sasa kazi ipo yeye ni muislamu.

Nanataka nibadilishe dini kwetu wana imani tosha walishakata niolewe na dini tofauti kwao juzi tumeenda hali ndio hiyo nimechoka kabisa.

Naombeni ushauri maana wakristo hawatamki ndoa ila nikipata waislamu wanadai ndoa fasta
hata miezi sita hafikii so niko njia panda hadi now.
Una hami na majini wewe naona..!
 
Mkuu kuna watu wamezaliwa katika familia za kipagani, lakini wakisha kukua na kujitambua wanaingia dini wanayoichagua wenyewe, sasa hapo unasemaje eti wameridhi kwa wazazi? Kuna sababu nyingi. Lakini kubwa ni kuaminishwa kuhusu maisha ya kiroho ambayo ndiyo faraja ya maisha ya baadae.
Kama wapo ni Wachache na mara nyingi wataegemea dini ya jamii inayowazunguka. Kama mpagani alizaliwa Pemba au Zanzibar(definetely kwa asilimia 99 atakua Muislam) lakini akizaliwa Mbeya au Njombe(kwa uhakika ziadi ya asimia 90 atakua Mkristo)!
Lakini mtoto wa Kipagani akizaliwa Mtwara,Morogoro,Pwani, Tanga, Masasi(maeneo yenye Uwiano unaokaribiana kati ya Ukristo na Uislam) basi huyo mtoto wa kipagani uwezekano wa kuwa dini mojawapo ya hizo ni 50/50!
 
Mrejesho sasa kama ulibadili din au laa na nn kilifuata.
 
hapo suluhisho wote muokoke muachane na dini muufuate uwokovu katika YESU KRISTO ndio mtaiona amani ya ndoa yenu. watu wa dini hawataweza kunielewa hapa zaidi watakejeli na kutukana.
Ushauri mzuri huu watu wa dini kwl hawatoelewa
 
Kwanza Dada tambua kuwa waislam huoa mke zaidi ya mmoja...hata kama atakwambia atakuwa na wewe tu huko mbeleni atajakwambia nataka niongeze mke wa pili, wa tatu n.k..
.kwa hiyo jiandae kisaikolojia kuishi maisha ya uke wenza..

pili talaka kwenye ndoa za kiislamu n kitu simple tu...
tatu angalia moyo wako unasema nini...kama unaona unaweza kuishi maisha mapya ya imani ya kiislamu na kuacha habari za Yesu Kristo..then you can decide. Yangu ni hayo tu.
 
Hakuna kitu hatari sana kama kucheza na Imani! MUNGU anasema tusiabudu miungu mingine... Inaonyesha jinsi gani MUNGU anavyokataa hii miungu.
Nakushauri baki na Imani yako... MUNGU atakupa wa kufanana na wewe huyo muislamu sio wako.
MUNGU ni mwema sana humpa mtu wake kile anachokitaka on time.
 
Back
Top Bottom