ni sawa akisubiri ndoa,navofahamu katika mafundisho ya dini zetu tunazo sali sidhani kama kuna dini au dhehebu amabalo linahamasisha au kufurahishwa na muumini wao kupata mtoto nje ya ndoa,Uzuri wakupata mtoto ndani ya ndoa ni kwamba unajihakikishia malezi ya mtoto na upendo baina ya wazazi wawili maana watakuwepo pamoja,ukipata mtoto nje ya ndoa hatari yake nikwamba kuna uwezekano mkubwa mtot kukosa malezi ya wazazi wote wawili maana nje ya ndoa ni ngumu wazazi wote wawili wawe wanakaa pamoja mda wote wa maisha yao ya malezi,
Nakitu kingine cha muhimu katika maisha watu wasichokijua nikwamba,sisi binadamu tunamapungufu kila mtu na kiasi chake,mnapokua kua wazazi wawili mnaishi pamoja husaidia katika malezi haswaa mtoto wenu asibebe mapungufu ya mmoja.Mfano mmoja wenu ni mlevi au kahaba na mwingine sio mlevi wala kahaba,endepo yule mlevi au kahaba akimlea mtoto peke yake,mtoto yule aliekuzwa katika mazingira ya ulevi na ukahaba ataona kumbe ni jambo lakawaida kuishi maisha ya ulevi na ukahaba maana aliyaona kwa mzazi,maana watoto huamini sana katika mambo yanayofanywa na wazazi wao kuliko yale yakuambiwa,huyapa uzito zaidi mambo wanayoyaona yakitendwa na kuyaiga kwa haraka.
Lakini kama wazazi wote wakiwepo wakimlea ni vigumu mtoto kuiga tabia upande mmoja yote na ni rahisi pia mzazi mmoja kumrekebisha mwenzake katika yale mapungufu yatakayojitokeza katika maisha yao,na hii kupelekea katika uboreshaji ya malezi ya mtoto yule maana ataona baba mlevi lakini mama anamkataza kila siku kumbe atagundua ulevi sio kitu kizuri,au mama anatabia za ukahaba lakini kutokana na uwepo wa baba anaona kila siku baba anaipinga vita ile tabia,hapo kichwani kwa yule mtoto anakua huku akigundua kumbe hili ni tatizo,sasa angekuwepo mzazi mmoja tuu kungekua hakuna wakumrekebisha mwingine na mtoto angeibeba hio tabia ya mzazi mmoja,kama haifai ndo angekua nayo na kama inafaa ndo hivo pia ishakua yake.
Siku hizi hata wizi,ujambazi na tabia nyingine za kihuni zinaongezeka kwa sababu watoto wengi asilimia kubwa ni wa nje ya ndoa na wazazi wale hawakuweza kuendelea kua pamoja,na hii kupelekea mzazi mmoja kushindwa kumthibiti mtoto katika malezi yanayovaa,na wakati mwingine mzazi huyo alieachwa na mtoto anakua katika frustrations na kupelekea hata yeye kuwatelekeza watoto au kutowajali haswa katika malezi maana hawezi kuwafatilia na wakati huo huo ahangaike na shughuli nyingine ukizingatia pia labda yupo katika mahusiano mengine sio ya baba wa yule wa mtoto wa kwanza,na hii kupelekea kutanga kwa watoto au kuanza kulelewa na watu wengine ambao ni ndugu na mwishowe watoto kujiingiza katika makundi yakihuni na tabia zisizofaa katika jamii,
Ndoa ndo kitu pekee amabcho kwa asilimia kubwa itakuhakikishia utaishi na mwenzako milele labda kwa mapenzi ya Mungu itokeee kutengana na hii kukuhakikishia kulea watoto wako mkiwa wawili, mzigo ukibeba peke yako ni mzito lakin mkibeba wawili hautakua na uzito sawa na ulivokua ukiubeba peke yako,Nadhnai utakua umeelewa hio kauli