Ni sahihi ndugu kugombania mirathi ya ndugu yake aliyemjengea nyumba mzazi wake na kuandika jina la mzazi wake kwenye umiliki?

Kisheria ni nyumba ya familia .ila kiungwana wanapaswa wakuachie ila unawezaje kuishi kwa kutegemea uungwana ww familia?
Mkuu issue ni kwamba Watanzania wengi sheria hatujui.

Kwa sheria za Tanzania hata nchi nyingi hasa hapa kwetu kitu alichofanya Ashraf hakimi wa morroco kwa hapa TZ ME wasijaribu maana TZ ndugu wa mama zetu wanaweza kurithi mali ya mama sheria inaruhusu. Yani mjomba mama mkubwa na mama mdogo.
Hata upande wa Baba zetu .
Ndugu zake kama Baba mkubwa , Baba mdogo na shangazi wanaweza rithi mali za ndugu yao.

Ila wengi wanaamua kuwaachia watoto tuu , ila wapo na wao wanaotaka mgao na wanagawana.

Kumuandikisha mzazi mali yako ni mbaya sana hasa ndugu wakiwa wokorofi na kama Baba kazaa na wanawake zaidi ya mmoja na mama kazaa na mwanaume zaidi ya mmoja .
 
Hapo ndio kwenye shida, ndugu mara nyingi huwa ni wakorofi sana
 
Inaumiza sana hii, mtu aliyepambana kujenga mali leo mnagawana
 
Kurudisha mpaka mzazi aamue kukurudishia .
Mpaka hapo hio nyumba kama umejenga sio ya kwako kwa 100%.
Ni ya mzazi maana ndio jina lake limeandikwa kwenye kiwanja.

Kurudisha mpk yeye aamue ndivyo sheria inavyosema mkuu.
Sijui kama kutakuwa na namana yoyote labda tafuta mwanasheria akushauri.
Ila kwa mfano ikatokea ndugu mmoja mwenye busara akaamua mali irudi kwa aliyeipambania kumjengea mzazi lakini ndugu wengine wakaghairi apo napo pia kutakuwa na shida?
 
Hamana namna swala la mali hapa Tanzania baada ya muusika kufariki ni swala ya familia mzima so familia lazima wakubaliane wote.
 
Ukimjengea kwenye kiwanja cha familia automatically hio itakua mali ya wote kwenye urithi.

ukitaka mali isihesabike kama ya familia ,mjengee bi mkubwa nyumba kwenye kiwanja chenye jina lako alafu muache akae,otherwise ukijenga kwenye kiwanja cha familia ndugu wanaweza kudai endapo siku huyo mzazi asipokuwepo na kisheria mtagawana sababu ipo kwenye kiwanja cha familia na wana hio haki .
UKimjengea mzazi eneo tofauti na pale alipoishi mwanzo ni kutengeneza psychological torture kwa mzazi, unamlazimisha kuishi ugenini kwa mda wake wa uhai ulosalia

Jenga apoapo, then saikolojikally ujiweke mbali na issue za mirathi
 
Kurudisha mpaka mzazi aamue kukurudishia .
Mpaka hapo hio nyumba kama umejenga sio ya kwako kwa 100%.
Ni ya mzazi maana ndio jina lake limeandikwa kwenye kiwanja.

Kurudisha mpk yeye aamue ndivyo sheria inavyosema mkuu.
Sijui kama kutakuwa na namana yoyote labda tafuta mwanasheria akushauri.
Yawezekana kwa kesi hii mzazi ameshatangulia mbele ya haki ndio maana wako ktk vuguvugu la mirathi.
 
Hapana kiwanja si cha familia bali kimenunuliwa na mtoto kisha kumuandikisha jina la mzazi je apo kutakuwa na mgawanyo wa mali au mpaka marehemu atoe wosia mali zirudi kwa mwanae??
Unaposema kiwanja siyo cha familia una maanisha nini? na unasema kiwanja kina jina la mzazi, unachotakiwa kujua Baba akifariki mali zake alizoziacha zinaolozeshwa zote, hizo mali zake azichunguzwi akapewa nanani, mfano huyo mzee nyumba angejengewa na Serikali je familia haitakiwi kurithi?
 
Mkuu issue ni kwamba Watanzania wengi sheria hatujui.

Kwa sheria za Tanzania hata nchi nyingi hasa hapa kwetu kitu alichofanya Ashraf hakimi wa morroco kwa hapa TZ ME wasijaribu maana TZ ndugu wa mama zetu wanaweza kurithi mali ya mama sheria inaruhusu. Yani mjomba mama mkubwa na mama mdogo.
Hata upande wa Baba zetu .
Ndugu zake kama Baba mkubwa , Baba mdogo na shangazi wanaweza rithi mali za ndugu yao.

Ila wengi wanaamua kuwaachia watoto tuu , ila wapo na wao wanaotaka mgao na wanagawana.

Kumuandikisha mzazi mali yako ni mbaya sana hasa ndugu wakiwa wokorofi na kama Baba kazaa na wanawake zaidi ya mmoja na mama kazaa na mwanaume zaidi ya mmoja .
Mkuu fafanua vizuri aiwezekani Baba mefariki kaacha mke na watoto kisha Baba mkubwa aende mahakamani halafu mahakama impatie ya urithi hii sheria ya wapi au Sheria ya baadhi ya kabila?
 
Unaposema kiwanja siyo cha familia una maanisha nini? na unasema kiwanja kina jina la mzazi, unachotakiwa kujua Baba akifariki mali zake alizoziacha zinaolozeshwa zote, hizo mali zake azichunguzwi akapewa nanani, mfano huyo mzee nyumba angejengewa na Serikali je familia haitakiwi kurithi?
Kiwanja si cha familia kwasababu hakijanunuliwa na mzazi, mtoto ndio aliyenunua lakini kwenye hati kaandikisha jina la mzazi. Pengine hati ya mauziano kina jina la mtoto na mmiliki ni mzazi
 
Nyumba yeyote iliyojengwa kwenye ardhi ya familia ni ya familia na siyo vinginevyo, na haijalishi ilijengwa kwa malengo gani itabaki kuwa mali ya famikia na lazima kwenye mirathi igawanywe
 
Hapana kiwanja si cha familia bali kimenunuliwa na mtoto kisha kumuandikisha jina la mzazi je apo kutakuwa na mgawanyo wa mali au mpaka marehemu atoe wosia mali zirudi kwa mwanae??
Kitu chochote unacho mpa mzazi na ukaandika jina lake basi ni cha mzazi na ni mali ya familia na lazima itagawanywa.. kosa lako ni kuandika jina lake na mzazi hakusema kwenye wosia shida ndipo inapo anzia
 
Na kama kiwanja ulinunua ila ukaandika jina la mzazi kwenye hati miliki nayo pia inakuwa mali ya familia??

Yan usizunguke sana kwa ufupi ni iv mwenye jina ndo mwenye mali
Km kiwanja umeweka jina la mama au baba ata km umenunua ww iyo ni mali ya familia
Ata km nyumba umejenga ww ila jina la hati umeandika mzee bas nyumba iyo ni ya familia

Na km baba mama wenunua kiwanja ila ww ukawajengea bado ni mali ya familia
Njia nzr na rahisi km unawapenda wazazi wako ni kununua kiwanja chako na kuwajengea ila majina yawe yako apo akuna atakae kuuliza wala kuhoji
 
Mkuu fafanua vizuri aiwezekani Baba mefariki kaacha mke na watoto kisha Baba mkubwa aende mahakamani halafu mahakama impatie ya urithi hii sheria ya wapi au Sheria ya baadhi ya kabila?
Mimi mwenyewe nilikuwa siamini nilipinga sana, Dada yangu ni mwanasheria aliniambia nilibishananae sana , nikaja kushuhudia.
 
Mkuu fafanua vizuri aiwezekani Baba mefariki kaacha mke na watoto kisha Baba mkubwa aende mahakamani halafu mahakama impatie ya urithi hii sheria ya wapi au Sheria ya baadhi ya kabila?
Mkuu ndo maana kwenye mali z marehemu wanaoshighulikia ni familia mzima. Ndo maana kunakuwa na kikao cha familia mzima upo apo.

Familia inamchagua mmoja yoyote kuwa ndo msimamizi wa mirathi.

Mimi niliyoyaona ni.

Baada ya Baba mmoja kufaliki na kuacha watoto wakibwa 4 na 3 wanandoa zao kabisa na wamesoma. Huyo baba walikuwa 5 kwao yeye alikuwa ni wa 2 wa kwanza alikuwa ni Mwanamke na aliolewa na mchaga. Ila wao kabila lao ni watu wa mgeta moro.

Baada ya Baba kufa na kuacha Watoto 4 na mke.
Dada yake mkubwa na wadogo zake walienda mahakamani na kudai sehemu ya mali za kaka yao.
Cha ajabu msimamizi wa mirathi wakamchagua mtoto wa kwanza wa Dada yao aliyeolewa na mchaga ndio awe msimamizi wa mirathi watu tulishangaa .

Na kesi ilisikilizwa Safi mahakamani.
 
Back
Top Bottom