Ni sahihi Rais Traore kukutana na maraisi huko Russia akiwa na bastola kibindoni?

Ni sahihi Rais Traore kukutana na maraisi huko Russia akiwa na bastola kibindoni?

Hii picha ya Rais Traore kukutana na Rais Maduro wa Venezuela huko Russia huku akiwa na Bastola yake inayoonekana wazi kabisa imejadiliwa sana.

Tena sio hivyo tu bali pia Traore ameshuka kwenye ndege huko Russia na akapokelewa hivyo hivyo akiwa na Bastola yake.

Kwa sisi wakali wa Diplomacy kutoka chuo cha diplomacy......tukutane hapa kujadili protocol

Je anachokifanya mwamba Traore .... tafsiri yake ni Nini???[emoji91][emoji91][emoji91]


View attachment 3330069

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Hilo ni toy tu. Hakuna risasi mule. Hivyo ni sehemu ya vazi lake. Wazungu huwezi kuingia kwenye maofisi yake na bunduki yenye risasi.
 
Nimeiuliza GROK AI, imenipa majibu haya:-

Je ni kweli Ibrahim Traore amefanikisha kujenga uchumi wa Burkinafaso kama inavyoandikwa kwenye page ya @africanhub_
Ili kupima ukweli wa madai kwamba Rais Ibrahim Traoré amefanikisha kujenga uchumi wa Burkina Faso kama yanavyoelezwa kwenye ukurasa wa @AfricanHub_
kwenye X, tunahitaji kuchunguza madai haya dhidi ya vyanzo vya kuaminika na data iliyopo.

:
1. Ukuaji wa GDP kutoka $18.8 bilioni hadi $22.1 bilioni
Madai: @AfricanHub_
inadai GDP ilikua kutoka $18.8 bilioni hadi $22.1 bilioni katika miaka miwili ya Traoré.
Uthibitisho: Kulingana na Ripoti ya Benki ya Dunia, GDP ya Burkina Faso ilikuwa takriban $22.92 bilioni mnamo 2023, ikiwa imepanda kutoka $21.8 bilioni mnamo 2022. IMF inakadiria ukuaji wa GDP wa 3.6% mnamo 2023 na inatarajia 5.5% mnamo 2024. Ripoti ya ISS Africa inasema kuwa uchumi unaweza kukua kwa wastani wa 8% kutoka 2025 hadi 2043, ikiwa mageuzi ya utawala yatatekelezwa. Hata hivyo, madai ya @AfricanHub_
kwamba GDP ilikua kutoka $18.8 bilioni hadi $22.1 bilioni ndani ya miaka miwili (2022–2024) inaonekana kuwa ya kupita kiasi kidogo, kwani takwimu za 2022 zinaonyesha GDP ilikuwa karibu $21.8 bilioni, sio $18.8 bilioni. Ukuaji hadi $22.1 bilioni au zaidi unawezekana, lakini takwimu za 2024 bado hazijathibitishwa kikamilifu na taasisi za kimataifa kufikia Mei 2025.
Hitimisho: Dai hili lina msingi, lakini takwimu ya mwanzo ($18.8 bilioni) inaweza kuwa chini kuliko ilivyo kweli. Ukuaji wa GDP umeonekana, hasa kutokana na kilimo, huduma, na uchimbaji madini, lakini haujafikia kiwango cha kushangaza kama inavyodaiwa.

2. Kukataa Mikopo ya IMF na World Bank
Madai:
Uthibitisho: Kuna ripoti nyingi zinazothibitisha kuwa Traoré ameelezea msimamo wa kupinga ushawishi wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na kukataa mikopo ya IMF na World Bank, akidai kuwa nchi inaweza kujitegemea. Hata hivyo, Benki ya Dunia bado inaendelea na miradi nchini Burkina Faso, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kilimo na miundombinu, japo uhusiano na taasisi hizi umepungua.

Hitimisho: Dai hili ni la kweli kiasi cha kuwa Traoré amechukua msimamo wa kupinga mikopo ya IMF na World Bank, lakini bado kuna ushirikiano mdogo na taasisi za kimataifa.

3. Kupunguza Mishahara ya Mawaziri na Kuongeza ya Wafanyakazi wa Umma
Madai: Traoré alipunguza mishahara ya mawaziri kwa 30% na kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma kwa 50%.
Uthibitisho: Ripoti kutoka MR Online na vyanzo vingine vinaunga mkono dai kwamba Traoré alikataa mshahara wa rais na akapunguza mishahara ya mawaziri, huku akiongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma. Hata hivyo, hakuna takwimu za kina zinazothibitisha asilimia husika (30% na 50%) katika vyanzo vya kimataifa kama IMF au Benki ya Dunia.

4. Kulipa Madeni ya Ndani
Madai: Traoré alilipa madeni ya ndani ya Burkina Faso.
Uthibitisho: Hakuna vyanzo vya kimataifa vinavyothibitisha moja kwa moja kuwa Traoré alilipa madeni yote ya ndani. Ripoti za Benki ya Dunia zinasema kuwa Burkina Faso inakabiliwa na changamoto za kufadhili deni lake, hasa kwenye soko la kikanda la WAEMU, ambapo viwango vya riba vimepanda hadi zaidi ya 9%. Hata hivyo, kuna madai kwamba Traoré alilipa deni la nje la $4.7 bilioni, kama ilivyoripotiwa na MEFeater na LN24, lakini hili halijathibitishwa na IMF au Benki ya Dunia, na linaweza kuwa limechangiwa na mapato ya dhahabu.
Hitimisho: Dai hili halijathibitishwa vya kutosha. Kuna uwezekano wa kupunguzwa kwa baadhi ya madeni, lakini madai ya kulipa madeni yote ya ndani yanaweza kuwa ya kupita kiasi.

5. Uanzishaji wa Viwanda vya Kuchakata Nyanya
Madai: Traoré alianzisha viwanda viwili vya kuchakata nyanya, vya kwanza nchini.
Uthibitisho: Vyanzo kama vile sokodirectory.com na malawiace.com vinathibitisha kuwa Traoré amewekeza katika viwanda vya kuchakata nyanya, na uzalishaji wa nyanya umeongezeka kutoka tani 315,000 mnamo 2022 hadi tani 360,000 mnamo 2024. Hii inaunga mkono juhudi za Traoré za kuimarisha kilimo na usindikaji wa ndani. Hata hivyo, hakuna ripoti za IMF au Benki ya Dunia zinazothibitisha moja kwa moja uanzishwaji wa viwanda hivi, japo Benki ya Dunia inaunga mkono maendeleo ya kilimo nchini.
Hitimisho: Dai hili lina msingi, kwani kuna ushahidi wa uwekezaji katika usindikaji wa nyanya, na takwimu za uzalishaji zinaunga mkono maendeleo haya.

6. Ufunguzi wa Mgodi wa Dhahabu na Kukomesha Usafirishaji wa Dhahabu Isiyosafishwa
Madai: Traoré alifungua mgodi wa dhahabu wa hali ya juu na kukomesha usafirishaji wa dhahabu isiyosafishwa hadi Ulaya.
Uthibitisho: Traoré amenationalize sekta ya dhahabu, akiunda kampuni ya umma inayomiliki 15% ya shughuli za uchimbaji na kujenga kiwanda cha kusafisha dhahabu, kama ilivyoripotiwa na BBC, Wikipedia, na ISS Africa. Kiwanda hiki kinatarajiwa kusindika tani 150 za dhahabu kila mwaka na kutoa ajira za moja kwa moja 100 na za moja kwa moja 5,000.
Hitimisho: Dai hili ni la kweli. Traoré amechukua hatua za kunationalize sekta ya dhahabu na kuzuia usafirishaji wa dhahabu isiyosafishwa, japo changamoto za kisheria na kiuchumi zipo.

7. Uanzishaji wa Kiwanda cha Pili cha Kuchakata Pamba
Madai: Traoré alianzisha kiwanda cha pili cha kuchakata pamba nchini.
Uthibitisho: MR Online inaripoti kuwa Traoré ameanzisha viwanda viwili vya kuchakata pamba huko Bobo-Dioulasso na Ouagadougou, na kuifungua tena kiwanda cha FASO FANI cha nguo.
Hitimisho: Dai hili ni la kweli, kwani kuna ushahidi wa uwekezaji katika usindikaji wa pamba, unaolenga kupunguza usafirishaji wa malighafi.

Uchambuzi wa Jumla
Madai yana msingi wa kweli katika baadhi ya maeneo, hasa kuhusu ukuaji wa GDP, uwekezaji katika kilimo (kama nyanya), na mageuzi ya sekta ya madini (dhahabu) na pamba. Traoré amechukua hatua za kukuza uhuru wa kiuchumi, kama kunationalize sekta za rasilimali na kupunguza utegemezi wa mikopo ya Magharibi. Ripoti za IMF na Benki ya Dunia zinaonyesha ukuaji wa uchumi wa 3.6% mnamo 2023 na matarajio ya 4–5% mnamo 2024–2025, pamoja na kupungua kwa umaskini wa hali ya juu kutoka 26.8% hadi 24.9% kutokana na ukuaji wa kilimo na huduma.
Hata hivyo, baadhi ya madai yanaweza kuwa yamechukua mkazo wa kupita kiasi au yanakosa uthibitisho wa kina:
Takwimu za ukuaji wa GDP zinaweza kuwa zimetia chumvi ($18.8 bilioni inaonekana chini kuliko takwimu za 2022 za $21.8 bilioni).
Dai la kulipa madeni yote ya ndani au deni la nje la $4.7 bilioni halijathibitishwa na vyanzo vya kimataifa na linaweza kuwa sehemu ya propaganda.
Mishahara ya wafanyakazi wa umma na mawaziri inaweza kuwa imebadilishwa, lakini asilimia husika (30% na 50%) hazijathibitishwa.
Zaidi ya hayo, Burkina Faso inakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijatajwa sana kwenye machapisho.
:
Usalama: Zaidi ya 40% ya eneo la nchi halidhibitiwi na serikali kutokana na mashambulizi ya kigaidi, na takriban watu milioni mbili wamekimbia makazi yao.
Mgogoro wa Kibinadamu: Takriban 10% ya wakazi wamekimbia, na kuna haja ya $877 milioni kwa msaada wa kibinadamu, ambayo haijakamilika.
Hali ya Kiuchumi: Licha ya ukuaji, umaskini unabaki juu (zaidi ya 40% wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa kitaifa), na uchumi unakabiliwa na hatari za usalama, msukosuko wa hali ya hewa, na changamoto za kufadhili deni.

Machapisho yaonekana kuwa na mwelekeo wa kukuza picha chanya ya Traoré, mara nyingi ukimlinganisha na Thomas Sankara, kiongozi wa mapinduzi wa Burkina Faso wa miaka ya 1980. Machapisho yao yana mwelekeo wa pan-Africanism na kupinga ushawishi wa Magharibi, ambayo yanawavutia wafuasi wengi, hasa vijana wanaotaka uhuru wa kiuchumi na kisiasa. Hata hivyo, machapisho haya mara nyingi yanapuuza changamoto za ndani za Burkina Faso na yanaweza kutia chumvi mafanikio ya Traoré ili kuimarisha umaarufu wake. Kwa mfano, kumudu Jenerali Langley bila kushughulikia maswala ya usalama na umaskini kunaweza kuwa na lengo la kumudu wapinzani badala ya kutoa picha kamili.

Hitimisho
Ni kweli kwa kiasi kwamba Ibrahim Traoré amefanikisha maendeleo ya kiuchumi huko Burkina Faso. uwekezaji katika kilimo (nyanya, pamba), na mageuzi ya sekta ya dhahabu yanayolenga uhuru wa kiuchumi. Hatua zake za kukataa mikopo ya IMF na World Bank na kunationalize rasilimali zimepata umaarufu mkubwa na zinaonyesha maendeleo katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo, madai mengine, kama kulipa madeni yote au ukuaji wa GDP wa ghafla, yanaweza kuwa yametia chumvi au yanakosa uthibitisho wa kina. Zaidi ya hayo, changamoto za usalama, umaskini, na migogoro ya kibinadamu zinasalia kuwa za msingi, na hazijashughulikiwa vya kutosha kwenye machapisho
.
 
Ni sahihi suala la usalama bado linaendelea kuwa kipengele katika miaka yake hii 2,

Lakini pia tukiangalia kwa mapana nazani suala la Usalama ni swala pana na ambalo linahitaji muda na si transition ya miaka 2.

Naomba tuangalie ni measure gani ambazo zimechukuliwa mpaka sasa ili kukabiliana na masuala ya kiusalama baada ya Kapteni Ibrahim Traoré,

I. Tangu wanajeshi wa Ufaransa kuondoka Januari 2023, serikali inayoongozwa na jeshi la Burkina Faso chini ya Kapteni Ibrahim Traoré imeimarisha uhusiano na Urusi. Takriban vikosi 300 vya wanamgambo wa Urusi viko chini kusaidia kulinda uongozi wa Burkina Faso.
Bado hali ya usalama haina improvement hivyo huo ushirika wake haujamsaidia. Juzi magaidi wameshambulia kambi ya jeshi na kuua wanajeshi, kuchoma silaha na kutoroka na silaha nyingine. Bado 40% ya nchi ina magaidi serikali haina umiliki nayo na shughuli za kiuchumi zimesimama.

Alichokikuta bado kipo vilevile, so hakukuwa na haja ya yeye kufanya mapinduzi maana hajabadili chochote kwa miaka miwili na nusu. Kama vipi nayeye apinduliwe, mbona yeye kampindua mtu aliyekaa miezi 8.
Juzi tarehe 12 yalitokea mashambulizi 8 ya kigaidi kwa siku moja. Mpaka leo mji wa Djibo uliotekwa siku hiyo haujapelekewa jeshi kukombolewa bado raia wako majumbani.

Traore kajitenga na kila nchi kubwa kasoro Urusi, ona Niger walivyo hawana bifu za kijinga na wengine. Jana hii
20250514_081352.jpg


II. Baada ya tukio la kigaidi lililotokea Agosti 24, 2024, katika eneo la Centre-Nord, Tukio hili lilipelekea raia kati ya 200 hadi 600 kuuwawa.

Hivyo mapema mwaka huu 2025, Burkina Faso, Mali na Niger zilitangaza kikosi cha pamoja cha askari 5,000 wa kupambana na ugaidi kutekeleza operesheni za kikanda, kwa matumaini ya kukabiliana vyema na tishio linaloongezeka.
Kati ya waliofanya mapinduzi wenya unafuu bila porojo ni Niger, yule jamaa aliyefanya mapinduzi ni mtu mzima, kazoea madaraka, sio kijana anayetafuta show off. Niger wamefanya improvement kwenye utawala na usalama ila hamtoi sifa sababu jamaa havai gloves na bastola kiunoni na kujitutumua anapambana na wazungu, badala ya kuwa mjanja mnafiki kufanya vitu chinichini.

Hilo jeshi la pamoja la 5,000 halipo hadi sasa. Nimekueleza hizo ni nchi masikini zote na zinapenda propaganda, maskini wakikutana ni mbwembwe zinatajwa utekelezaji sawa na hakuna.

Walitaja kuunda jeshi kama wasiwasi wa kuvamiwa na ECOWAS kuondolewa madarakani kipindi Nigeria inaandaa vuguvugu. Hayo mambo ya kupambana na ugaidi not of their serious concern kuliko madaraka yao.

Traore ni Makonda aliyechangamka, camera nyingi ila hatua za maana hamna na damage kwa nchi yake katika ushirikiano wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom