Naomba twende taratibu mkuu haraf tuangalie kwa miaka hiyo miwili, Is he a Leader worth following?
Baadhi ya hatua muhimu za kwanza za Traoré alizichukua ilikuwa ni kurejesha udhibiti wa maliasili za Burkina Faso. Hii ni baada ya kushindwa kufikia Makubaliano kuhusu ununuzi upya wa migodi ya dhahabu ya Boungou na Washington kutoka kwa kampuni ya Uingereza ya Endeavor Mining.
Hii ilipelekea serikali yake kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha kitaifa cha kusafisha dhahabu. Badala ya kusafirisha madini ghafi sasa Burkina Faso inaweza kuuza hadi tani 150 za dhahabu iliyosafishwa kila mwaka kwa viwango vya soko, Hence mapato yote yanabaki zaidi ndani ya nchi.
Kabla Traore hajafanya mapinduzi, mwaka 2022 mgodi wa Wahgnion uliingia hasara kwenye operations. Mgodi wa Boungou uliingiza hela ila migodi yote hii ni open pit na haina dhahabu kivile na ndio maana inauzwauzwa hovyo.
Migodi hiyo iliuzwa kutoka kampuni ya Endeavor kwenda Lilium Mining.
Kutokana na usalama mbovu kama nilivyokueleza 40% ya Burkina Faso ina magaidi basi logistics ni ngumu hivyo kampuni mnunuzi (Lilium) ikawa inakula hasara ikashindwa kumalizia makubaliano ya malipo na haijawa interested kuendelea haijafanya uchimbaji hata 3 yrs. Ikabidi badala yake Endeavor ikubaliane na serikali ya Burkina Faso kuchukua migodi ile na ndio italipa sasa.
Kwahiyo serikali ya Traore ilitakiwa kumalizia kiasi fulani wakakubaliana $30 million. Hata wasipolipa sasa, makubaliano ya madini deni halifi sio biashara ya nyanya ile kampuni za madini huwa haziji locally.
Miaka ya 2023 hadi sasa ndio kidogo uzalishaji umeongezeka kwenye migodi hiyo miwili, hata hivyo bado kuna migodi mingine ambayo inazalisha dhahabu zaidi na haimilikiwi na serikali.
Kwahiyo serikali imenunua migodi miwili kwa sababu waliouziana wamegombana wakaamua deni limalizwe na serikali.
Investing in the Nation:
Kapteni Traoré ametumia utajiri unaozalishwa ndani ya nchi yake ikiwa ni pamoja na mapato ya dhahabu kwa maendeleo ya Taifa lake. Kwanza kabisa,
I. Banking.
Alianzisha Benki ya Posta inayomilikiwa na serikali ili kuhakikisha mifumo ya malipo kwa idadi ya watu, kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa kifedha.
Sijui kuhusu hili, good move.
II. Viwanda vya nguo.
Burkina Faso ni mzalishaji mkubwa wa pamba barani Afrika na iliyoorodheshwa ya kumi duniani, iliona msaada wa kisheria na uwekezaji katika sekta yake ya nguo.
Hivyo ilipelekea kufungua Kiwanda cha pili cha pamba kinachomilikiwa na serikali, na uagizaji wa nguo za mitumba kutoka nje ulipigwa marufuku ili kuongeza uzalishaji wa ndani.
Sijui kuhusu hili, good move.
III. Kilimo.
Zaidi ya matrekta 400 ya kisasa, pamoja na mbegu, mbolea, na vifaa vya kilimo, yaligawiwa kwa wakulima wa ndani.
Design ya yale matrekta niliyoona kwenye picha hata bilioni 10 za Kitanzania hazifiki. Not a big deal wakati more than 2 million farmers wamekimbia mashamba yao kisa ugaidi.
Matokeo yake ni yapi?
- Uzalishaji wa nyanya uliongezeka, kutoka tani 315,000 mwaka 2022 hadi tani 360,000 mwaka 2024 (+14%).
- Uzalishaji wa mtama ulipanda, kutoka tani 907,000 mwaka 2022 hadi tani milioni 1.1 mwaka 2024 (+21%).
- Uzalishaji wa mpunga ulikua, kutoka tani 280,000 mwaka 2022 hadi tani 326,000 mwaka 2024 (+16%).
Kila kitu mwaka 2022 kilisimama, ndio maana unalinganisha growth VS huo mwaka tu haulinganishi na miaka mingine, wala hutopata meaningful continuos growth.
Na ukichunguza hiyo pattern utakuta production ya miaka mingine inaelekeana kasoro 2022.
Why?
➡️2022 kulitokea mapinduzi January akaondolewa Roch Marc Kabole na akaingia Paul Damiba.
➡️2022 September Traore akafanya mapinduzi.
Baada ya Damiba kufanya mapinduzi kulikuwa na detention, fukuto, fukuzafukuza, patrols kwa miezi kadhaa hali haijatulia. Institutions zilibadilika na mambo yote yalilala kwanza. Baada ya Traore kupindua hali ikawa vilevile kwa muda.
Kwahiyo 2022 ni black year kwa Burkinabe ukizingatia effects za COVID-19 duniani kiuchumi na supply chain.
Tuje kwenye Miundombinu na Usafirishaji:
Miradi muhimu ya miundombinu pia ilianza,
- Uwekaji lami wa barabara ambazo hazikuwa na lami hapo awali nchini kote.
- Uboreshaji wa uwanja wa ndege wa pili wa kimataifa, Ouagadougou-Donsin, Uwanja huu unatarajiwa kuhudumia zaidi ya abiria milioni 1 kila mwaka baada ya kukamilika mwishoni mwa mwaka huu 2025.
Projects ambazo yeyote angefanya. Lami si inawekwa na kila Rais, hata yeye akiondoka sahivi, kesho atakuja mwingine ajenge lami.
- Kufufua shirika la ndege la taifa kupitia ununuzi wa ndege mpya.
Kanunua ndege moja, zilikuwepo mbili wakafunga operations. So kama kafugua shirika maana yake wanazo ndege tatu, mbili chovu sana na moja used kutoka China. Unless otherwise, nipe habari.
Tumalizie na Mafanikio ya Kiuchumi na Kisiasa:
I. Ukuaji wa Pato la Taifa.
Pato la Taifa la Burkina Faso lilikua kutoka takriban $18.8 bilioni hadi $22.1 bilioni-karibu ongezeko la 17%.
II. Mishahara ya Umma.
Mishahara ya mawaziri na wabunge ilipunguzwa kwa 30%, wakati mishahara ya wafanyikazi wa serikali iliongezwa kwa 50%.
III. Usimamizi wa Madeni.
Deni la ndani la nchi lililipwa lote kabisa.
IV. Lugha na Vyombo vya Habari.
Vyombo vya habari vya Ufaransa vilipigwa marufuku, na Kifaransa kikaondolewa hadhi yake kama lugha rasmi.
Lugha haiondolewi kwa matamko. Nenda taasisi zao uone kama hawatumii Kifaransa. Au shule zao hela za kununua vitabu vya lugha nyingine na kubadili mitaala na kufundisha upya walimu wanayo?
Kwahiyo wanatumia kugha gani kwa sasa mkuu mbona Foreign Minister wao hutoa machapisho kwa Kifaransa.
V. Mabadiliko ya Kidiplomasia.
Baada ya mapumziko ya miaka 31, Burkina Faso sasa imeanzisha upya ubalozi wake na ukaribu na Urusi.
Traore kaua diplomasia ya nchi kuliko kujenga. Kaja na shutma na kujitenga na Western countries anataka ajifungie na Russia pekee au na China.
Rais yeyote mjanja anaishi na nchi zote, Burkinabe kuna vitu wanavyo na Warusi wala Wachina hawanunui. China iko mbali nao kuliko Ulaya na walikuwa na biashara na Ulaya, tena biashara ya raia wake wala sio serikali. Kazira wakati ni maskini.
VI. Ushirikiano wa Kikanda.
Kupitia Mali na Niger, Burkina Faso ilianzisha kwa pamoja Shirikisho la Mataifa ya Sahel, Ni shirikisho pekee linalofanya kazi duniani leo.
Shirikisho uchwara. Wote wana instability kila muda patrols wanaogopa kupinduana, wote wana magaidi, wote wametengwa na jumuiya za kikanda, wote ni maskini, wote hawana intra-trade za kusaidiana. Hakuna mwenye economic advantage zaidi ya mwingine, Tufanye Burundi na Rwanda zijitenge sasa zitafaana nini wakati huku ndizi, kule ndizi, huku kahawa kule kahawa.
##############
Tukianzia na sababu za Traore kufanya mapinduzi na kipi hasa Burkina Faso wanataka. Alifanya mapinduzi yale sababu kuu ikiwa ni ukosefu wa usalama. Traore alimpindua Damiba ambaye alikaa madarakani kwa miezi saba pekee ambayo haikutosha kufanya mabadiliko makubwa.
Kwa miaka miwili na nusu aliyokaa Traore ameshindwa kurudisha hali ya kiusalama kuwa na unafuu, aliingia akakuta nchi 40% iko chini ya magaidi na hadi sasa 2.5 yrs later 40% ya nchi iko chini ya magaidi.
Kaingia madarakani late 2022 ila mpaka sasa 20% ya shule zimefungwa na 20% ya vituo vya afya vimefungwa. Tatizo kuu la Burkina Faso ambalo anashindwa kupiga hatua kidogo mpaka sasa hata hayo mengine akiacha nayo kabisa, raia watamshukuru akileta
usalama
Kisai