Ni sahihi Rais Traore kukutana na maraisi huko Russia akiwa na bastola kibindoni?

Ni sahihi Rais Traore kukutana na maraisi huko Russia akiwa na bastola kibindoni?

Ungetuwekea ushahidi wa haya unayoyaandika ingekuwa bora zaidi.
Mkuu kama hukubaliani na nilichoandika ni kazi yako kupinga kwa kuonyesha ushahidi, sio kazi yangu kujiwekea ushahidi mwenyewe kwa sababu sijipingi.
 
Huyu dogo natamani sana nione uhakiki wa hata kimoja alichokifanya, mnakera sana na mapambio ya kumsifu.
Huko kwake Kuna mtandao huru kama huu wa JF nipitie na kusoma kinachosemwa na raia wake, pale ambapo wanatoa maoni bila kuogopa hayo magwanda yake?
Hana lolote huyo dogo. Umaarufu wake ni zao la social media tu.

Habari nyingi sana kumhusu yeye ni za uongo uongo au zilizotiwa chumvi nyingi.

Tuliambiwa eti alikataa mwaliko wa Trump kuhudhuria uapisho wake 🤣. Na watu wakaamini tu bila kujua kwamba hilo ni rahisi sana kulithibitisha.

Sasa hivi kwenye mitandao kuna videos zikimwonyesha akiongea Kiingereza.

Sina uhakika sana kama ni yeye. Nadhani ni video za kutengenezwa.

Sidhani kama yuko fluent kivile kwenye Kiingereza.

Kawachota akili wajinga na wapumbavu ambao wanaamini kila kitu kuhusu yeye.

Ana cult following ya wajinga, wapumbavu, na majuha.

Anazunguka na hicho kibastola chake huku kavaa magwanda utadhani ni mlinzi wa getini.

Naye watampindua tu kwa staili ile ile aliyoingia nayo madarakani.

Hizi zama zama social media zina wajinga na wapumbavu wengi sana.

Wao wakiona kitu chochote tu mtandaoni, basi wanakiamini mazima.

He is a hype job!
 
Wewe unafikiri hao marais wenzake waliovaa suits (akina Puttin) hawana bastola? Waulize watu wenye chembe chembe za masuala ya ulinzi na usalama watakwambia. Ukweli ni kwamba hao wote wana bastola kwenye makoti yao, hawatembei kizembe wameficha mapanga ya kizungu ndani ya koti.

Sikuhizi watu waliozoea kutembea na silaha za moto hawatembei na silaha kiunoni/pajani, huwa wanazichomeka ndani ya koti ambalo limeshoneshwa vizuri kwa ndani. Kikinuka utawaona wanaingiza mkono ndani ya koti kama vile wanajikuna kwenye mbavu[emoji38]

Traore ni kama waafrika wenzake ambao wakimiliki magari wananing'iniza ufunguo wa gari kwenye ruksi ya suruali, lakini wenzetu wanaoyaunda hayo magari hawaning'inizi funguo za gari kwenye ruksi/mikanda ya suruali.
Hahaaa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo hata tukikwambia siyo sahihi itakusaidia nini? We endelea kukamua mawese huko kazuramimba
 
Inasemekana mengi ni uwongo, deep fakes na AI generated images and videos japo baadhi ya mambo ni kweli. Al Jazeera waliliongelea hili kipindi fulani. Dogo amepata cult following na ameleta msisimko sana kwamba sasa Afrika angalau inaongelewa katika muktadha wa kimajumui na ameleta mvuvumko wa kujikomboa na kujitegemea. Na hili ni jambo jema!
Hiki kiswahili kimekaa Kama AI generated 😀
 
Hii picha ya Rais Traore kukutana na Rais Maduro wa Venezuela huko Russia huku akiwa na Bastola yake inayoonekana wazi kabisa imejadiliwa sana.

Tena sio hivyo tu bali pia Traore ameshuka kwenye ndege huko Russia na akapokelewa hivyo hivyo akiwa na Bastola yake.

Kwa sisi wakali wa Diplomacy kutoka chuo cha diplomacy......tukutane hapa kujadili protocol

Je anachokifanya mwamba Traore .... tafsiri yake ni Nini???[emoji91][emoji91][emoji91]View attachment 3330069

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Wenyeji wake wanasemaje?
 
Self diffence🪝
 
Yeye Iko wazi inaonekana, ila zipo njemba ambazo nchi zao ziko na falsafa kama za Russia chuma ziko ndani ya Makoti tena double double Hadi magotini hahh
 
Kama mataifa ya Afrika yakijielewa siku moja, labda tunaweza kufika mahali
Huyu ni mmoja katika nchi zaidi ya 50.
Mjitafakari
 
Back
Top Bottom