Ni sahihi TBC kuonyesha michuano ya CAF Champions League?


Hapo utakuta ulilipia ili uone halafu rafiki yako akakupigia kukuraarifu TBC wanaonesha bure kabisa. Roho mbaya hapo unatamani upige ukuta ngumi.
 
Hujawahi kupitisha mwezi bila kulipia Kisha unasema hujaona Cha maana aisee!!
 
siwezi kuangalia mpira kupitia tbc bora tuu nilalee
 
Kama vipi TBC nayo irushe ligi kuu, kama ni mitambo hatakosa, watangazaji mahiri inayo
 
Anauliza mdau wa X au wauliza wewe...?

TBC ni televisheni ya umma, ipo huru kuonesha kila mchezo uwe wa CAF, UEFA, FIFA n.k kama tu ikikidhi vigezo vya vibali...
ikidhi tu hivyo vigezo tupate burudani kupitia tv ya umma, tumechoka na utemi wa azam ni ghali sana kifurushi chake kwa mwezi
 
Hivi kuiona Tbc sio lazima uwe umelipia king'amuzi husika? Sijawahi kufuatilia
 
Mipira ya Africa ya ndani yote TV za Taifa zina haki ya kuonyesha mipira yote sema wale Dstv walikua wanatoa rushwa kubwa kwa baadhi ya Nchi zisiwe zinaonyesha ili wao wauze wiki iliyopita pana wakuu wawili wameacha kazi kwa kashfa hiyo SA Mult Choice sema hii haki wengi walishaisahau wanaona sio haki yao maana FIFA na CAF wanatoa pesa kusapoti tuone Mpira kupitia TV ya Taifa..
 
mabepari yanataka yahodhi matangazo yote ya mpira tv za taifa zisioneshe
 
Ulitaka tuangalie kupitia kwenye domo lako?
 
Ukifikiria hivyo sana utajijuwa wewe!
Utaanza kuuliza kwanini yule ana mke mzuri kuliko Mimi wakati wangu namhudumia kuliko yeye..
Utaanza kujiumiza kwanini yule ana gari nzuri wakati Hana kazi kama yangu?!
Acha roho mbaya ndugu....
 
Inategemea na leseni inatolewaje.

Mfano Epl mwenye leseni Kusini Jangwa la sahara ni Dstv, mtu yoyote atakayeonesha inabidi achukue leseni kwao.

Kama Leseni Ya Tanzania anayo Azam basi TBC wamenunua kwa Azam, kama Michuano haina Leseni exclusive basi wote Wawili wanaweza kununua Caf na Waka onesha.

Mwenye kauli ya mwisho ni Caf wenyewe na sio Azam.
 
Acha Watu Washuhudie Pira Safi La Dar Young Africans Kwanza.

Baadae Ndio Tutarudi Kuzungumza Haki Za Matangazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…