Ni sawa kufanya tohara? Kwanini muumba aliweka govi?

Ni sawa kufanya tohara? Kwanini muumba aliweka govi?

storyteller

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2014
Posts
1,511
Reaction score
1,844
Ni dhahiri kila mwanaume huzaliwa akiwa na uume wenye ngozi inayofunika kichwa cha uume(govi). Katika tanzania kuna makabila kadhaa ambayo unaweza mkuta kijana hajatahiriwa na wala asiwe na wasiwasi kulinganisha na makabila mengine kijana asipotahiriwa inaonekana ni tatizo na anaweza pata fedheha.

Sasa nimekua nikijiuliza maswali nini chanzo cha binadamu(wanaume) kuona haja ya kutahiriwa ikiwa mwanaume anazaliwa akiwa na govi, je ni sawa kufanya tohara, na kama ni sawa(kwa mujibu wa vitabu vya dini) kwanini muumbaji aliweka govi.

Nini faida ya kuwa na kutokuwa na govi.

Nina hakika wana jamvi mnaweza nisaidia kwa maswali haya machache, na nimeuliza kwa kuwa sijawahi kuexperience ukiwa na govi inakuaje maana hadi natambua uume una kazi mbili(kukojolea na kuwekea mbegu za uzazi katika uke), nlikua nishafanyiwa tohara.

Wasalaam.
 
Anhaa..unazungumzia govi a.k.a mkono wa sweta, je hapo ulipofanyiwa tohara una mapungufu yoyote? Nguvu za uume zimepungua?

Binaadam anapozaliwa a azaliwe na nywele, hunyolewa na huota tena
Hukatwa kitovu,
Huzaliwa na Hilo govinder( mtoto wa kiume ) na kulipunguza nahisi ni kustaarabika tu, pia ha kupunguza chochote Ila govi linahifadhi uchafu
 
Sababu za mwanzo kabisa za kutoa govi ninazozijua mimi ni sababu za kiimani zaidi, ambapo mtu wa kwanza kabisa kukata govi alikuwa ni mzee Ibrahimu katika kitabu cha Mwanzo 17;10, pale Mungu alipofanya naye agano na kumuahidi kuwa atampatia uzao mwingi, na tena mzee Ibrahimu hapo kabla alikuwa akiitwa Ibraimu na baada tu ya kukatwa govi akabatizwa jina jipya akaitwa Ibrahimu, yeye alikatwa govi yake akiwa na umri wa miaka tisini na tisa (99). Hili ni agizo la Mungu Mwenyewe kwa Ibrahimu na kizazi chake chote na watumwa wake wote. Ila kwa siku za hivi karibuni nimewahi kusoma sehemu fulani ikitoa sababu za kutahiriwa ikiwa ni masuala ya kiafya zaidi. Niishie hapa.
 
Mtu wa kwanza kukata govi hakuwa Ibrahim
 
Warumi 2 : 25 - 29.

Kwa maandiko ukiacha na swala la usafi.
Kutahiriwa kuna maana kama unatii sheria.
Warumi 2 : 25 - 29.

25 Kutahiriwa kuna thamani tu iwapo unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, umekuwa kama hukutahiriwa. 26 Kwa hiyo kama watu ambao hawakutahiriwa wanatimiza maagizo ya she ria, je, Mungu hatawahesabu kuwa kama waliotahiriwa? 27 Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanatii sheria watawa hukumu ninyi mlio na Maandiko ya sheria nakutahiriwa lakini mna vunja sheria. 28 Kwamaana Myahudi wa kweli si yule anayeonekana kwa dalili za nje, wala tohara ya kweli si kitu cha kimwili. 29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ya kweli ni jambo la moyoni, jambo la kiroho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa jinsi hii anapata sifa kutoka kwa Mungu, wala si kutoka kwa wanadamu.
 
Kutahiri....ni afya...sababu wanaume wengi ni wachafu hasa huko mahali.....lakini pia ni saikolojia tu ...wanaume tuna amini kutahiri ni ushujaa, pia heshima pia kuonekana smart na kujiamini mbele ya wanawake ktk tendo la ndoa....ila kimsingi kama mwamaume ataacha hiyo kitu awe msafi sana, pia asivurugwe na hizo saikolojia za ushujaa au aibu! Kutahiri kwa rohoni ni kibiblia, kimwili ni kiafya tu kwa wahanga wa uchafu.
 
Back
Top Bottom