Ni sawa kufanya tohara? Kwanini muumba aliweka govi?

Ni sawa kufanya tohara? Kwanini muumba aliweka govi?

Warumi 2 : 25 - 29.



Kwa maandiko ukiacha na swala la usafi.
Kutahiriwa kuna maana kama unatii sheria.
Warumi 2 : 25 - 29.

25 Kutahiriwa kuna thamani tu iwapo unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, umekuwa kama hukutahiriwa. 26 Kwa hiyo kama watu ambao hawakutahiriwa wanatimiza maagizo ya she ria, je, Mungu hatawahesabu kuwa kama waliotahiriwa? 27 Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanatii sheria watawa hukumu ninyi mlio na Maandiko ya sheria nakutahiriwa lakini mna vunja sheria. 28 Kwamaana Myahudi wa kweli si yule anayeonekana kwa dalili za nje, wala tohara ya kweli si kitu cha kimwili. 29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ya kweli ni jambo la moyoni, jambo la kiroho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa jinsi hii anapata sifa kutoka kwa Mungu, wala si kutoka kwa wanadamu.
Hallelujah we mkuu mleta mada kama unalo katolewe usione aibu
 
Ni dhahiri kila mwanaume huzaliwa akiwa na uume wenye ngozi inayofunika kichwa cha uume(govi). Katika tanzania kuna makabila kadhaa ambayo unaweza mkuta kijana hajatahiriwa na wala asiwe na wasiwasi kulinganisha na makabila mengine kijana asipotahiriwa inaonekana ni tatizo na anaweza pata fedheha.

Sasa nimekua nikijiuliza maswali nini chanzo cha binadamu(wanaume) kuona haja ya kutahiriwa ikiwa mwanaume anazaliwa akiwa na govi, je ni sawa kufanya tohara, na kama ni sawa(kwa mujibu wa vitabu vya dini) kwanini muumbaji aliweka govi.

Nini faida ya kuwa na kutokuwa na govi.

Nina hakika wana jamvi mnaweza nisaidia kwa maswali haya machache, na nimeuliza kwa kuwa sijawahi kuexperience ukiwa na govi inakuaje maana hadi natambua uume una kazi mbili(kukojolea na kuwekea mbegu za uzazi katika uke), nlikua nishafanyiwa tohara.

Wasalaam.
Ndio maana kuna Agano Jipya na Agano la Kale
 
Daah govinda ni mtihani, cubemate wetu alikua analala na suruali 7bu ya mkono wa sweta. You loose confidence kwenye halaiki.
Ila sasa iringa naona wanadondosha hizo sweta
 
Kutahiri....ni afya...sababu wanaume wengi ni wachafu hasa huko mahali.....lakini pia ni saikolojia tu ...wanaume tuna amini kutahiri ni ushujaa, pia heshima pia kuonekana smart na kujiamini mbele ya wanawake ktk tendo la ndoa....ila kimsingi kama mwamaume ataacha hiyo kitu awe msafi sana, pia asivurugwe na hizo saikolojia za ushujaa au aibu! Kutahiri kwa rohoni ni kibiblia, kimwili ni kiafya tu kwa wahanga wa uchafu.
Asante.
 
Sababu za mwanzo kabisa za kutoa govi ninazozijua mimi ni sababu za kiimani zaidi, ambapo mtu wa kwanza kabisa kukata govi alikuwa ni mzee Ibrahimu katika kitabu cha Mwanzo 17;10, pale Mungu alipofanya naye agano na kumuahidi kuwa atampatia uzao mwingi, na tena mzee Ibrahimu hapo kabla alikuwa akiitwa Ibraimu na baada tu ya kukatwa govi akabatizwa jina jipya akaitwa Ibrahimu, yeye alikatwa govi yake akiwa na umri wa miaka tisini na tisa (99). Hili ni agizo la Mungu Mwenyewe kwa Ibrahimu na kizazi chake chote na watumwa wake wote. Ila kwa siku za hivi karibuni nimewahi kusoma sehemu fulani ikitoa sababu za kutahiriwa ikiwa ni masuala ya kiafya zaidi. Niishie hapa.
Kwaiyo Suleiman alikuwa govi Dah.
 
Kama nikilifanyia usafi wa kina nikiliacha ni kosa? Ukikata kucha zinaota nyingine hata nywele zinaota lakini govi halioti lingine. Niruhusuni niliache usafi nitajitahidi. Au kuna sababu nyingine?
 
Kichwa cha uume kinapofunikwa na ngozi kinatengeneza uchafu ambao si mzuri naunaharufu mbaya sana

Pia uwezekano mkubwa wa kupata HIV

Wakati wa tendo kichwa cha uume kina vipele fulan hivi amaizing so kinapoingia ukeni kinamkuna mwanamke vzuri tofauti na govi
 
Kwaiyo Suleiman alikuwa govi Dah.
Hapana hakuwa na govi, sababu babu ya baba na mababu zake tangu huko mwanzo wala babu yake yeye hajulikani kama atakuja kuzaliwa, yaani mzee Ibahimu, ambaye ni wa kwanza kutahiriwa alikatwa hiyo govi, baada ya hapo umekuwa ni utaratibu wao, na kama mtu asingetahiriwa basi angakufa!! Kwa hiyo Suleiman alitahiriwa kama ilivyo desturi ya wa Israel wote mkuu
 
Yesu alivyokuja duniani alitengua yote yaliyokuwa Agano la kale na likaja Agano Jipya. That means sio lazima asili ibakie na asili yake, wanadamu kila kukicha tunapata akili
Unachokisema ni kweli ndugu, sababu ya kutahiriwa kwa Ibrahimu ilikuwa ni ishara ya agano kati ya Mungu na mtumishi wake Ibrahimu, katika agano jipya imeegamia kiimani zaidi yaani kutahiriwa moyo, tangu hapo kutahiriwa kwa mwili kumekuwa si kitu tena, ila ni kwa mwenye Imani thabiti juu ya mafundisho ya Jesu Kristo kupitia mtume Paulo
 
Hapana hakuwa na govi, sababu babu ya baba na mababu zake tangu huko mwanzo wala babu yake yeye hajulikani kama atakuja kuzaliwa, yaani mzee Ibahimu, ambaye ni wa kwanza kutahiriwa alikatwa hiyo govi, baada ya hapo umekuwa ni utaratibu wao, na kama mtu asingetahiriwa basi angakufa!! Kwa hiyo Suleiman alitahiriwa kama ilivyo desturi ya wa Israel wote mkuu
Kwani Suleiman na Ibrahim Nani wa Kwanza kuzaliwa au nabii gani wa kwanza kati ya hao.
 
Kichwa cha chini chenyewe huwa hakitaki kukaa kwenye mfuko huwa kinaomba mfuko uondolewe kipate hewa safi
 
Kwani Suleiman na Ibrahim Nani wa Kwanza kuzaliwa au nabii gani wa kwanza kati ya hao.
Ibrahim ndiyo wa kwanza kuwepo duniani kabla ya Suleiman, Suleiman amezaliwa na mfalme Daudi, na mfalme Daudi amezaliwa na Yese, Yese amezaliwa na Obedi na Obedi amezaliwa na Boazi,

huyu Boazi alimwoa Ruth ambaye hapo kabla aliolewa na mmoja wa watoto wa mama mmoja wa kiirael aliyeitwa Naomi, huyu Naomi alifiwa na mumewe katika nchi ya ugenini na baada ya muda watoto wake wawili wa kiume pia wakafa akabakia na wakweze wawili ambao mmoja wao ndiyo huyu Ruth aliye chanzo cha mfalme Daudi babaye na mfalme Suleiman.

Ibrahimu ndiye baba wa Isaka, Isaka baba wa Esau ambaye jina lingine huyu Esau anaitwa Edomu na pia ni baba wa Yakobo ambaye jina lake lingine anaitwa Israel.

Tangu hapo vizazi vingi vimepita mpaka kuja kuzaliwa mfalme Suleiman.
 
Back
Top Bottom