Ni dhahiri kila mwanaume huzaliwa akiwa na uume wenye ngozi inayofunika kichwa cha uume(govi). Katika tanzania kuna makabila kadhaa ambayo unaweza mkuta kijana hajatahiriwa na wala asiwe na wasiwasi kulinganisha na makabila mengine kijana asipotahiriwa inaonekana ni tatizo na anaweza pata fedheha.
Sasa nimekua nikijiuliza maswali nini chanzo cha binadamu(wanaume) kuona haja ya kutahiriwa ikiwa mwanaume anazaliwa akiwa na govi, je ni sawa kufanya tohara, na kama ni sawa(kwa mujibu wa vitabu vya dini) kwanini muumbaji aliweka govi.
Nini faida ya kuwa na kutokuwa na govi.
Nina hakika wana jamvi mnaweza nisaidia kwa maswali haya machache, na nimeuliza kwa kuwa sijawahi kuexperience ukiwa na govi inakuaje maana hadi natambua uume una kazi mbili(kukojolea na kuwekea mbegu za uzazi katika uke), nlikua nishafanyiwa tohara.
Wasalaam.