Ni sawa kuwasiliana ukweni kabla ya kuoa?

Ni sawa kuwasiliana ukweni kabla ya kuoa?

Kifulu

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
557
Reaction score
2,064
Wakuu hivi kama umepeleka barua kwa mwanamke umejibiwa mahari ni kiasi Fulani

Je ni sawa kuwasiliana nao labda mama mkwe kumjulia Hali au baba mkwe kumsalimu ni sawa au miyeyusho??
 
Wakuu hivi kama umepeleka barua kwa mwanamke umejibiwa mahari ni kiasi Fulani

Je ni sawa kuwasiliana nao labda mama mkwe kumjulia Hali au baba mkwe kumsalimu ni sawa au miyeyusho??
Hapana, utafanya hayo sana hapo baadae. Utulie
 
🤣Kitamramba🥴
Hatoamini nakwambia..... Yaani mi sa hivi sijui naenda mwaka wa pili ama watatu sijawahi kumpigia Cha shemeji,mama mkwe sijui nani ...hakuna kabisa .... Kilichonikuta kujifanya "family" maana ni tumekuwa mtaa mmoja tumesoma Shule Moja tumetengana chuo tu ..so mabraza zake walikuwa washikaji kinomanoma ,masister zake ...kilivyoniramba ...nikasemaa eeeeh kisu kimegusa mfupa....
 
Ngoja siku wafiwe wakupe msiba usimamie mazishi mpaka chakula pesa zikutoke mpaka uishiwe nauli ya kurudi kwenu ukweni sio pakupazoea
Unashirikishwa mpaka harusi ya kirembwe upande wa bibi mza mama dadayake na mama mdogo ....hatari sana ....
 
Inategemea.

Kuna wakwe ambao wanauza Binti Zao. (Kuchukua Mahari) Hao kikawaida hupaswi kuwazoea kwa Sababu za kiitifaki.

Alafu kuna Wakwe ambao hawawauzi mabinti Zao. Hawa hawana shida.
Hao ni Kama Watibeli.
Sisi mth akioa binti yetu anakuwa sehemu yetu. Hatuwezi kumuuza Binti yetu na Wala hatuwezi mnunulia kijana wetu.

Tamaduni zote za watu wanaouza Binti Zao zinakataza mazoea Ukweni.

Tofauti na tamaduni zisizouza binti Zao.

Mtu aliyekuuzia Binti ili awe Mkeo hawezi kuwa kama mzazi wako Dunia iende irudi.
It was a business na siku zote biashara ni biashara tuu
 
Hatoamini nakwambia..... Yaani mi sa hivi sijui naenda mwaka wa pili ama watatu sijawahi kumpigia Cha shemeji,mama mkwe sijui nani ...hakuna kabisa .... Kilichonikuta kujifanya "family" maana ni tumekuwa mtaa mmoja tumesoma Shule Moja tumetengana chuo tu ..so mabraza zake walikuwa washikaji kinomanoma ,masister zake ...kilivyoniramba ...nikasemaa eeeeh kisu kimegusa mfupa....
Mwanaume kuwa busy na familia yako hapo kwako at least mwanamke ndiyo awe mwepesi kwenda kutembelea wazazi wako ila siyo marazote... sometimes
 
Back
Top Bottom