Ni sawa kwa baba au mama kuwaficha watoto kuwa ana ugonjwa wa (UKIMWI)

Ni sawa kwa baba au mama kuwaficha watoto kuwa ana ugonjwa wa (UKIMWI)

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Habari zenu Wana Jamii forums

Wazazi wengi wanaishi na ugonjwa wa UKIMWI kwa Siri bila watoto wao kujua na wanatumia ARV kwa siri chumbani. Na wengi wao wanaogopa kueleza Hali zao za Afya kwa familia wakihofia kudharaulika,sababu watoto now days shuleni wanajifunza UKIMWI unatokana na ngono zembe.
 
Ni sawa na pia inawezekana isiwe sawa .
Hapa inategemea umri wa watoto na utayari wao wa kupokea taarifa ngumu kama hiyo. Inahitaji maandalizi

Usipokuwa makini unaweza kuwaathiri ki saikolojia na wakashindwa kukua vyema na kufanya vizuri shuleni.
 
Aisee Kwa upande wangu naona ni sawa kabisa kuwaficha watoto kuhusu kuumwa ukimwi wengi wataathirika sanaa kisaikolojia siku wakijua
 
Ugonjwa wa mtu ni siri yake na dactari wake huna sababu ya kuwaambia watoto labda kama n watoto watu wazima
 
Acha waje kujua wenyewe, hii kitu huwa ni mbaya sana hasa watoto wakifahamu wakiwa katika umri mdogo.
 
Back
Top Bottom