SoC02 Ni sawa umenizaa, lakini umefupisha maisha yangu

SoC02 Ni sawa umenizaa, lakini umefupisha maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
Jioni ya jana nikiwa natoka katika harakati zangu za kila siku niliamua kufaya mazoezi kwa kutembea kwa miguu tokea kazini hadi nyumbani tofauti na nilivyozoea malanyingi huwa napanda usafiri wa umma asubuhi na jioni kwasababu sina chombo binafsi cha usafiri.

Nikiwa nakatiza katika mitaa karibu kidogo tu na nyumbani nikaona kuna zogo kubwa sana nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa. Kauli nilizokuwa nazisikia tangu nikiwa mbali zilinifanya nisogee karibu nikajionee mwenyewe kuna tukio gani maeneo yale.

Mala wengine wanasema "haiwezekani hawa lazima wafungwe!" Wengine wanasema "mwenyekiti nae afungwe anawafuga sana washenzi kama hawa."
Kiukweli sikuelewa, nilipata hamasa zaidi ya kwenda kushuhudia kitu gani hasa kimetokea.

Kufika naona Mama Jacqueline na mumewe wamezingirwa na umati mkubwa wa watu, wengine wakiwapiga na wengine akizuia wasipigwe basi ni vurugu mtindo mmoja. Huku Jacqueline ameshikwa na mama mmoja aliyekuwa anajitahidi kumfuta machozi na kumwambia asilie Mungu atamsaidia.

Nilimuangalia Jacqueline kwa umakini zaidi nikaona hayupo sawa, damu zinachuruzika miguuni, nikamuuliza yule mama aliyesimama nae, "vipi huyo mtoto amepatwa na jeraha gani?"
Akanijibu kwa kifupi,

"Yani we acha tu kaka yangu Dunia hii ina maajabu mengi."

Nikamalizia kusema
"na haya ndio maajabu yenyewe."
Japo bado nilikuwa sijaelewa ni kitu gani hasa kilichotokea.

Niliamua kumpandisha sketi yake kidogo yule mtoto ili nione jeraha lenyewe linalotoa damu, yule mama ndio akaniambia

"Hapana, usimfunue zaidi hautaona. Huyu mtoto amelawitiwa na baba yake wa kambo."

Nilishangaa sana
"Sasa mtoto amefanyiwa ukatili kama huu na bado mpo hapa! Ebu tumpeleke hospitali haraka iwezekanavyo."

Nilisaidiwa na watu wachache kumkimbiza mtoto Jacqueline hospitali huku tukiwaacha watu wengine pale ili wafanye taratibu za kuwafikisha watuhumiwa katika kituo cha polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.

Kufika hospitali, walikataa kutoa huduma yoyote hadi wapate PF3 au report maalumu kutoka kituo cha polisi inachothibisha kutokea kwa tukio lililopelekea majeraha kwa mtoto yule.

Tumeambiwa hilo ni takwa la kisheria hivyo hawawezi kufanya vile tunavyotaka sisi, kwani vinginevyo watakuwa wanakiuka sheria na maadili ya kazi au taaluma yao kwa ujumla. Ilibidi tuendelee kusubiri tu, hakuna namna.

Wazazi walifikishwa kituo cha polisi na report maalumu ikaandaliwa na kuletwa hospitali. Lakini kipindi tunasubiri huduma nilipata nafasi ya kuzungumza na Jacqueline mtoto wa miaka nane (08).

Mtoto huyu alinisimulia mambo mengi sana, mambo ya kutisha kiasi ambacho kama ningeyajua hayo kabla ya kumleta hospitali pengine na mimi ningetakiwa kwenda jela kwa kosa la mauaji. Kwa hasira nilizonazo nahisi ningepiga wale wazazi wake kiasi hata cha kuua kwa ushetani waliokuwa wakiufanya kwa mtoto Jacqueline.

Jacqueline amenileza kuwa, baba yake mzazi alifariki tangu akiwa na miaka mitatu. Mwaka mmoja baadae mama yake aliolewa na huyu baba mwingine tajiri aliyekosa akili wala chembe ya ubinadamu. Kwa uchungu sana Jacqueline ananiambia.

" Baba alianza kuniingilia ukeni muda mrefu tangu mwishoni mwa mwaka wa juzi. Ilikuwa ni kipindi cha likizo shuleni. Nilimwambia mama lakini mama alinipiga na kuniambia niache ujinga, baba hawezi kufanya hivyo, labda nimefanya na mtu mwingine huko mtaani arafu namsingizia baba. Baba nae alinipiga eti akidai namdharirisha."

Jacqueline anaendelea kusema,
"Kuna siku baba alinivuta chumbani kwake, mama alikuwa ametoka lakini alirudi ghafra na kumkuta baba akiwa juu yangu, huku akiniziba mdomo nisipige kelele. Niliishiwa pumzi nikahisi nakufa.

Siku ile nilijua sasa mama atakuwa upande wangu kunitetea lakini hakufanya hivyo. Nilirejea chumbani kwangu, baadae mama nae akaja chumbani kwangu na kunisihi nisimwambie mtu yoyote kwani nitamtia aibu yeye pamoja na mume wake yaani baba yangu wa kambo."

Jamani Dunia ina mambo hii. Ndugu msomaji endelea kusoma tafadhali. Jacqueline anaendelea kueleza
"Mama ameniambia, huoni hapa tunaishi kwenye nyumba ya kifahari, tunakula vizuri, tunalala pazuri, tuna magari mazuri ya kutembelea!! Huoni mwanangu kama ukithubutu kumwambia mtu yeyote basi baba yako atafungwa? Lakini pia hata sisi hapa ndugu zake watatufukuza kwasababu sina mtoto nae, wewe ndio mtoto wa pekee. Mama alinisihi zaidi nivumilie."

Duh! Anaendelea kusema
"Kuna siku nilimwambia Madame Glory, mwalimu wetu wa darasa ambae ni rafiki na mama yangu. Nilidhani atawaambia walimu wenzake ili wajue namna ya kunisaidia lakini hakuwaambia. Jioni tulivyotoka shule alinipeleka kwa mwenyekiti wa mtaa lakini walishauriana waachane na mambo hayo, kwani hayawahusu, mimi waliniambia tu nisiwe na wasiwasi, watamuita baba ili wamkanye aache tabia mbaya lakini hata hivyo sikuona mabadiriko yoyote niliendelea kuteseka tu."

Dah! Hapo niligundua uwezo mkubwa wa ufahamu wa mtoto Jacqueline, kwani anasimulia kwa umakini kama vile anayeongea ni mtu mzima, kumbe ni mtoto wa miaka nane tu.

Jacqueline anazidi kutokwa machozi, anakohoa kidogo kisha anaendelea kunisimulia,
"Leo hii ndio baba ame.... amenilalia na kuniingiza kwa nyuma."
Hapo akaanza kulia kwa uchungu sana, nikakosa namna ya kumbembeleza.

Kisha kwa sauti ya chini na kwa shida sana akaniambia maneno ya mwisho niende nikawaambie wazazi wake,
"Mama yangu, mwanao nakufa, najua sitapona. NI SAWA UMENIZAA, LAKINI UMEFUPISHA MAISHA YANGU. Mwambie na baba kuwa naenda kumwambia Mungu juu ya ubaya wote mlionifanyia"

Nurse mmoja alikuja kunitoa kwenye chumba alicholazwa Jacqueline akisubiri matibabu. Aliniambia PF3 imeshafika hivyo tunaomba utoke nje ili tuanze kumuhudumia.

Hazikupita hata dakika tatu nurse yuleyule alikuja kuniambia, mgonjwa wetu amepoteza maisha. Niliumia kupita kiasi kana kwamba mimi ndio baba halisi wa mtoto Jacqueline.

Dunia ina watu wa ajabu sana. Kuna mambo yanaumiza sana, lakini acha niishie hapa. Nashindwa kuendelea kuandika mengi zaidi kuhusu maisha ya mtoto Jacqueline.

Ni kweli watoto wengi katika jamii zetu wanapitia magumu kama haya. Jamii tushirikiane kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.

BILA SHAKA UMEVUTIWA NA STORY HII YENYE MAFUNZO, HIVYO NAOMBA KURA YAKO TAFADHALI.
______________________
Mwandishi: Mr. George Francis
Simu: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Upvote 11
very sad(RIP Jacqueline ) Jamii kwa ujumla elimu inatakiwa tubadili mtazamo sisi huku wengi kuchukua hatua hawawezi tumejaa uoga wa kipumbavu na kujikuta tunaharibu zaidi na zaidi. Kwa kweli jamii ya watanzania tunatakiwa kubadilika.
 
Kiukweli inaumiza sana, jukumu la kuwalinda watoto dhidi ya ukatili ni letu sote
 
very sad(RIP Jacqueline ) Jamii kwa ujumla elimu inatakiwa tubadili mtazamo sisi huku wengi kuchukua hatua hawawezi tumejaa uoga wa kipumbavu na kujikuta tunaharibu zaidi na zaidi. Kwa kweli jamii ya watanzania tunatakiwa kubadilika.
Well said. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuwalinda watoto kwa namna iliyo bora bila kuogopa chochote
 
Honestly nimeshindwa malizia kusoma..Moyo umeniuma nikawawaza wanangu wako likizo kwa dada wa mke wangu (shemeji yangu) ..Sasa hiv napiga simu watoto warud nyumban..Dunia hii haina hata sababu ya kumuamini yeyote yule..😭😭😭😭
 
Imagine mama mwenyewe wa mtoto huyu, amejua juu ya ukatili anaofanyiwa mwanae lakini tamaa za kukosa mali za mwanaume mwenye mali zinamfanya ashindwe kufichua maovu anayofanyiwa mtoto. Kiukweli inaumiza sana, watu wanaweza kuskip kusoma kutokana na urefu wa story but in reality kuna kikubwa cha kujifunza kwenye story hii.
 
Ndio maana mimi nikipata mtoto yeyote wa kike ama kiume, ndio itakuwa mwisho wa ndugu yeyote wa kiume kukaa nae kwangu. Watakuwa wakija na kurudi siku hiyo hiyo. Mtoto wangu kwenda kwa ndugu na kulala huko haitotokea..
 
Akili ya mwanamke inawaza pesa tu
 
Imagine mama mwenyewe wa mtoto huyu, amejua juu ya ukatili anaofanyiwa mwanae lakini tamaa za kukosa mali za mwanaume mwenye mali zinamfanya ashindwe kufichua maovu anayofanyiwa mtoto. Kiukweli inaumiza sana, watu wanaweza kuskip kusoma kutokana na urefu wa story but in reality kuna kikubwa cha kujifunza kwenye story hii.
Ku skio kusoma si kwasababu ya urefu wa habar ila ni kwakua kama mzazi unaweza ukashindwa kuvumilia kusoma maana unapata picha kana kwamba ni mwanao ametendewa ukatili huo..Inaumiza sana mkuu
 
Ku skio kusoma si kwasababu ya urefu wa habar ila ni kwakua kama mzazi unaweza ukashindwa kuvumilia kusoma maana unapata picha kana kwamba ni mwanao ametendewa ukatili huo..Inaumiza
Ku skio kusoma si kwasababu ya urefu wa habar ila ni kwakua kama mzazi unaweza ukashindwa kuvumilia kusoma maana unapata picha kana kwamba ni mwanao ametendewa ukatili huo..Inaumiza sana mkuu
It's true
 
very sad(RIP Jacqueline ) Jamii kwa ujumla elimu inatakiwa tubadili mtazamo sisi huku wengi kuchukua hatua hawawezi tumejaa uoga wa kipumbavu na kujikuta tunaharibu zaidi na zaidi. Kwa kweli jamii ya watanzania tunatakiwa kubadilika.
Jamii zinapaswa kubadilika sana, hali inatisha kiukweli matendo ya ukatili ni mengi mno
 
Ndio maana mimi nikipata mtoto yeyote wa kike ama kiume, ndio itakuwa mwisho wa ndugu yeyote wa kiume kukaa nae kwangu. Watakuwa wakija na kurudi siku hiyo hiyo. Mtoto wangu kwenda kwa ndugu na kulala huko haitot

Ndio maana mimi nikipata mtoto yeyote wa kike ama kiume, ndio itakuwa mwisho wa ndugu yeyote wa kiume kukaa nae kwangu. Watakuwa wakija na kurudi siku hiyo hiyo. Mtoto wangu kwenda kwa ndugu na kulala huko haitotokea..
Ni kweli watu siku hizi hawaaminiki lakini nasi wazazi tunatakiwa kuwa makini sana na watoto wetu. Katika tukio kama hili mama wa mtoto anahusika kwa asilimia zaidi ya 90% katika kuficha ukatili uliopelekea kifo cha binti yake
 
Hivi nyie wanaume mna nini lakini.

Inaumiza.

I voted to you
Thank you so much madame.

Lakini pia kina mama niwaombe kuwa makini na hawa watoto wenu, tamaa ya pesa na mali isiwe sababu ya kuficha maovu yanayofanywa na kina baba kwa wototo wenu. Jamii inapaswa kuamka na kupiga vita ukatili.
 
Back
Top Bottom