Ni sawa Waziri Chana kukutana na Balozi wa Urusi leo wakati tunapokea ugeni wa Makamu wa Rais wa Marekani?

Ni sawa Waziri Chana kukutana na Balozi wa Urusi leo wakati tunapokea ugeni wa Makamu wa Rais wa Marekani?

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,555
Reaction score
6,972
Ni kweli uliowazi kuwa mataifa makubwa haya matatu ya Marekani ,Urusi na China yanakimbizana na kupishana Afrika kijaribu kuongeza ushawishi wao kisiasa na kuongeza ushirikiano pamoja na kukuza biashara.

Ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani ni hauko mbali na malengo hayo. Kila mtu atakuja kwa wakati wake fursa zake

Alichofanya Waziri Chana leo kukutana na Balozi wa Urusi nchi siku ambayo ugeni wa makamu wa Rais wa Marekani ni kitendo cha makusudi kabisa dhidi ya ugeni unaokuja.

Sisi sera yetu hatufungamani na upande wowote tangu awamu ya kwanza hata sasa ndio maama tulijitenga na kura ya kutaka Urusi ichukuliwe hatua kutokana na vita yake dhidi ya Ukraine. Hivyo hakuna haja ya sisi kujaribu kutia doa kuonesha kuwa tuko na fulani hata ujuo wako sio muhimu.

Ukisoma CV ya Waziri Chana amesoma na kufanya kazi Urusi ( kwa mwaka 1) hivyo inaweza kuwa ana mlengo wa kisiasa unaofanana na huko na hivyo kutopendezwa na ujio wa mgeni wetu huyu. Ushindani wa kuharibiana na muendelezo wa 'cold war' tuwaachie wao wenyewe sisi tubaki kusikiliza na kutoonesha kufungamana na upande wowote

Tangu lini Urusi wamekuwa na shauku na mchezo wetu wa Soka hapa Tanzania mpaka leo wakafika uwanja wa Taifa na kuonana ma waziri wa Michezo uwanjani
 
Balozi wa Urusi hata Marekani yupo, hakuna cha ajabu hapo
Katika siasa kila tukio lina maana yake. Taswira inayowekwa kwa timing hiyo ni ipi?
 
Acha mambo yaende sambamba, yaani lifanyike hili halafu hili lisubiri tutachelewa sana.
 
NI SAWA, haiingii akilini shughuli nyingine zisimame Kwa sababu anakuja makamu wa Rais, isingewezekana wote wakaenda kumpokea au wasipoenda wapumzike.
 
Kwani kwenda kwake kunazuia huo Bibi wa Marekani kupokelewa???!!
Hapana , mfano kwenu Mzazi anajiandaa kupokea ugeni halafu na wewe wakati wanajiandaa, wewe unapokea mgeni wakati Mzazi wako yuko juu juu na ugeni wake!
 
Balozi wa Urusi hata Marekani yupo, hakuna cha ajabu hapo
Hilo tu ni pigo la kisaikolojia kwa Marekani na ushindi kwa Urusi,anaeandamwa na beberu za ulaya na Amerika🤔
 
Ukisoma CV ya Waziri Chana amesoma na kufanya kazi Urusi ( kwa mwaka 1) hivyo inaweza kuwa ana mlengo wa kisiasa unaofanana na huko na hivyo kutopendezwa na ujio wa mgeni wetu huyu...
Ebu acheni ujinga!. Kwani tukipata ugeni wa Marekani, ndio tusimamishe wageni wengine wote?!. Kwani Marekani ndio nani?.
P
 
Ebu acheni ujinga!. Kwani tukipata ugeni wa Marekani, ndio tusimamishe wageni wengine wote?!. Kwani Marekani ndio nani?.
P
Sawa Sawa Mjomba lakini mkubwa wako anavyojiandaa ugeni na wewe katikati unapokea ugeni ku antagonise ugeni wa mkubwa wako ni sawa?
 
Back
Top Bottom