Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Mwanza miambani wananoishi. Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu.View attachment 2378247
Duuuu hatari Sana Kama maeneo ya Igogo na Mabatini hiviiii
 
Izimbya ni sehemu ambayo ipo tofauti na maeneo mengi ya mkoa wa Kagera pakame, migomba haina afya, ardhi haina rutuba, huduma za kijamii zipo kww manati, nilistaajabu sana kwa waliouzunguka mkoa huo watakubaliana na mimi
 
Kijiji cha Chimendeli, wilaya ya Bahi Mkoa WA Dodoma.


Sijui kule watu Wanaishi vipi. Unaweza Kudhani uko Somalia au Afghanistan.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Dodoma ni hatari ,kuna vijiji vinapatikana shortcut (mpwapwa to Iringa road)
Imagine hadi wakiona gari wanakimbia,ilibidi tushuke kwanza tuwauulize maswali ya hapa na pale kuhusu maji,chakula maana Hamna mazao kabisa na vumbi linatimka muda wote ,watoto wamebabuka hatari unahisi hata wakipiga maji hawatakati,kiswahili pia shida
 
Habari za muda huu wanajf.

Nchi yetu Ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?
Kijiji cha Bugamba Kigoma vijijini mwambao wa ziwa Tanganyika
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.
Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.View attachment 2378247
Hahah..hi ngoma ni kishiri kama sikosei
 
Ilunde Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi. Kijiji kipo Porini, Kilomita 70 toka makao makuu ya Wilaya ya Mlele. Hakuna network wala nini na ni Porini hasa. Sijui walifuata nini kule.
Tanzania hii ni kubwa sana nashangaa watu kujilinganisha na Rwanda, na Kenya kimaendeleo wakati hizo nchi zinaingia mara mbili kwa Tanzania
 
Back
Top Bottom