Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Habari za muda huu wanajf.

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?
Uwe unataja Kijiji, kata , wilaya , na mkoa ili watu waelewe unazungumzia eneo gani , sasa kyagata ndio nini na ndio wapi?
 
Dodoma ni hatari ,kuna vijiji vinapatikana shortcut (mpwapwa to Iringa road)
Imagine hadi wakiona gari wanakimbia,ilibidi tushuke kwanza tuwauulize maswali ya hapa na pale kuhusu maji,chakula maana Hamna mazao kabisa na vumbi linatimka muda wote ,Vitoto vimebuka hatari unahisi hata wakipiga maji hawatakati,kiswahili pia shida
[emoji1][emoji1]

Dodoma ninadhani ndio mkoa unaongoza Kwa mazingira magumu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Nilipanda mlima uluguru nikakuta waluguru huko juu Tena wanavijiji vyao Hali ya hewa ilikuwa nzuri ila huduma za kijamii Hadi uteremke mlima, binafsi nilishuka miguu inatetemeka na maumivu makali mno. Mpaka Leo nawashangaa watu Kule wanavyoishi
 
Habari za muda huu wanajf.

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?
Upareni kule juu au Lutindi Korogwe
 
Back
Top Bottom