Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Na kule jangwani mi nawaonaga hawana akili sawasawa watu
 
Pole sana Mwanza ndio ya pili kwa Dar kwa uwingi wa magari hapa Tz.
 
Nilifika Gonja Mawole huko Same sitasahau kuna sehemu tulifika ikawa mwisho wa gari. Kupanda na kutelemka ndio ikawa kazi ilikuwa wakati wa mvua udongo wa mfinyanzi utelezi ni hatari. Nilijiuliza sana kwamba hivi hawa wapare kuishi huku walimkosea nini Mungu ?
 
Mwanza visiwa vya ziwa Victoria Zilagura,Nkome,Kasalazi na Gozba.Kuna wafanyabiashara wa Dagaa,bia na petrol pesa Mtu anaweka Kwenye mifuko na haibiwi. Gesti zimejengwa na mabanzi baadhi ya visiwa network shida
Huko visiwa vya Ziwa viktoria hawa jamaa wanaoishi uko wako free sana ni kama wapo kwenye dunia yao wenyewe pekeyao. Hawana habari na yanayoendelea kwingineko. Na wapo wengi tu wanaishi uko lakin hata mwanza mjini hawapajui na ukitaka kukosana mwambie ahame uko visiwani. Ngono inapigwa nje nje kama ngoma mtaji mkubwa wa akinadada ni kujichubua tu ela inakuja yenyewe!
 
We jamaa muyovozi iwe mbaya kuliko shunga? Anyway mwaka gani apo
 
Mimi ni zamani kidogo mwaka 2012 uwenda kwa Sasa Kuna maendeleo..
Kwa kipindi kile hali ilikuwa mbaya Sana..Kijiji kinaitwa UFANA Ni BABATI vijijini huko..
 
Wapare ndio zao kujificha milimani, Uende Chome, Vuje, Vunta, Tae, Bwambo ni milimani haswa wakati maeneo mazuri yapo.
 
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]mlendaaaa!!noooooo
Mboga za majani Bora kabisa kwangu ni mlenda/ msusa , unafata mchicha , Tembele, Chinese , kabeji ,. .... mboga za majani ambazo sitaki hata kuziona ni kisamvu
 
Umenikumbusha kisiwa kiitwacho Ghana, ndani ya Ziwa Victoria, katika Wilaya ya Ukerewe.
Kuna watu mbali mbali wa ajabu kule. Kuna kila aina ya biashara kule, kuanzia ufusker na mambo mengine mengi. Upande wa biashara, products nyingi zinazopatikana kule ni Made in Kenya. Sijuhi, labda Kenya si mbali kutoka Ghana.
Ili uishi kule inabidi uwe na roho ngumu. Ili ufike kule inabidi upande yale maboti makubwa makubwa yaliyofungiwa bati juu kwa ajili ya kujikinga na jua & mvua. Stand kuu ya kwenda kule inaitwa Kakukuru.
Aiseee, tembea uone!
 
Kakukuru kata ya mulutilima...hapo beach ya kakukuru ndio stendi ya boti nyingi za kwenda visiwani huko (last time nilienda kakukuru 2020)...Siku za kufunga makambi huko visiwani wenyewe wanaita kutegeruka hapo kakukuru usafir wa kwenda nansio inakua ni patashika
 
Halafu huwa wana mbwembwe hao....akiwa vijijini kwao huko akiulizwa hivi flani huwa unaishi wapi? Anajibu kwa madaha mwanza😂😂
 
Dodoma pazuri mjini TU pale na Kondoa pale mjini vijijini hukoo ni shida kwanza kuna sehemu nilienda wanatumia maji Yale kama maziwa hivi hata kwetu Kijijini hayapo kabisaa
Ndio maana ukiowa mwanamke wa kirangi ni rahisi sana kuhadaika na maisha ya mjini wengi wao wanazaliwa wanakulia kwenye maisha magumu chakula chao kikubwa ni ugali na nsanza ( majani yaliyokaushwa yanakaangwa halafu unatafuna kama karanga)
 
Mimi ni mwenyeji sana japo kwenye mawe ni mgeni kabisa na sijawahi shawishika kukaa huko juu maana kwa haraka haraka tu ni kwa watu masikini sana kwa hali ya nyumba wanazoishi. Pia mtu mwenye pesa hawezi jenga huko
 
Mm nilifika sehemu moja inaitwa NYINGWA unapita matombo
 
Kijiji cha Chimendeli, wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.

Sijui kule watu Wanaishi vipi. Unaweza Kudhani uko Somalia au Afghanistan.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Hiki kijiji niliona juzi channel 10 walikuwa wakifuatilia watu wanaotorosha watoto na kuja kuomba omba(mawakala)nilikuwa na mke wangu tunacheki jamani,jamani mke wangu akasema pale wapi nikamwambia ile wilaya ya Bahi Dodoma alichoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…