Kyambamasimbi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 762
- 1,597
- Thread starter
-
- #901
Ni dharau kubwa Sana mkuuUkisoma humu ndani unagundua kua watanzania wanapambana sana kujitafuta , juhudi na risk wanazochukua kuitafuta kesho njema ni kubwa, be blessed
Halafu mtu anakuja kutukana kua waafrika wavivu ,shenzi kabisa
Hatari mkuu na kiswahili Chao utaskia jaaa! Mjomba nawe!!Sio mchezo unakutana na viluguru vifupi na matenga ya ndizi vichwani
Pakoje mkuu, japo nilikua napita pana jua kali na upepo huo hatari.Pale SINGIDA mjini.
Hatarii mkuu Kuna watu wanaishi milimani Turiani ni hatarrr mpaka unajiuliza sijui walifikaji sijui walidondoka? Hata ukiumwa hakuna barabara hakufikiki kirahisi Ni Kama kisiwa.Nimezunguka sehemu kibao watu wanaishi sehemu ambazo ukifika
Unajiuliza walifikaje huko na kuanza maisha milimani
Wengine ukiongea nao wanakuambia enzi za nguvu kazi
Watu ndiyo walipoanza kukimbiaa
Ova
Hahahahaha nimecheka sanaKuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.
Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.
Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.
Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.
Hahaha noma sansWewe kilimanjaro una maanisha Moshi, njoo same na mwanga ndiyo utajua hujui. Watu huku wamekauka unaweza kuwapasua kuni na ukapikia maharage yakaiva haraka kuliko stima
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.
Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.
View attachment 2378247
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Vijiji vya njiani ukiwa unapita kwenda mikoani unakuta mtu anatembea kuelekea uelekeo ambao ww huoni nyumba
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Vijiji vingi vya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu utashangaa wasukuma Sijui walifata nini huko, unakuta kijiji hakina umeme Wala maji. Yaan Maji yao wanachimba mabwawa kipindi cha mvua Maji yanatuama humo basi ng’ombe na binadam wote ndo mnakunywa Maji hayo!! Maji Kama maziwa kuna wachawi huko sijapata ona!! Wanga wananza kuwanga saa moja jioni!! [emoji2][emoji2]
Huko unakuta msukuma ana ng’ombe 50-100 ila anakula ugali na dagaa wa mwanza wale gredi ya mwisho kabisa ambao huwa kwaajili ya vyakula vya Kuku!![emoji2][emoji2] huko ikifika saa 12 jioni tembo kutoka serengeti wanaingia kijiji kula miwa[emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kwa konje, handeni iko ndani ndani masaa sita kwa baisikeli kutoka makuyuni. Kila nyumba ina kibwengo
Mbarali hakuna sehemu za ajabu kote kunafikika kirahisi, mazingira rafiki watu kuishi na fulsa za kumwaga.Sion Mbarali ikitajwa.
Ukisikia mapanga na mishale jua ni mkoa wa Mara tuIko kijiji kipo mkoa gani mzee.
Acha uongo mwakaleli huduma za kijamii zote zipo baridi ikikushinda wewe siyo kigezo Cha kushindwa kuishi wengineMwakaleli- Tukuyu Mbeya. Aisee baridi lilinishinda pale Mwax sec.
Tunda kimasihara[emoji1787][emoji1787]Kijiji kingine ni mpyagula, kwa mbele kuna wasukuma wengi miaka ile wali na kambale mkubwa sana ilikua ni mia tano tu, mwenyeji wangu aliponiona kama nina mawazo akajadili na mke wake wakamwita binti mdogo wa mke wake aje anifariji chumbani na binti alikua mwanafunzi nilishangaa sana sitosahau hiko kisa
[emoji16]Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
Kwa nn mkuuNguserosambu, Ngorongoro,na Loliondo, Nadhani hata Mungu hana muda wa kwenda huko