Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Nimezunguka sehemu kibao watu wanaishi sehemu ambazo ukifika
Unajiuliza walifikaje huko na kuanza maisha milimani
Wengine ukiongea nao wanakuambia enzi za nguvu kazi
Watu ndiyo walipoanza kukimbiaa

Ova
Hatarii mkuu Kuna watu wanaishi milimani Turiani ni hatarrr mpaka unajiuliza sijui walifikaji sijui walidondoka? Hata ukiumwa hakuna barabara hakufikiki kirahisi Ni Kama kisiwa.
 
Kuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.

Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.

Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.

Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.
Hahahahaha nimecheka sana
 
Huu uzi ni toka 2022 ni mzuri unafurahisha na kuhuzunisha pia..nilipoanza page 1 nikajikuta namalizia zote 46.mpk sasa zilipofikia...HAKIKA TANZANIA NI KUBWA NA WATU WANAISHI MBALI SANA TENA KATIKA MAZINGIRA YA KUSHANGAZA.🙌🙌
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.

Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.

View attachment 2378247
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Vijiji vingi vya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu utashangaa wasukuma Sijui walifata nini huko, unakuta kijiji hakina umeme Wala maji. Yaan Maji yao wanachimba mabwawa kipindi cha mvua Maji yanatuama humo basi ng’ombe na binadam wote ndo mnakunywa Maji hayo!! Maji Kama maziwa kuna wachawi huko sijapata ona!! Wanga wananza kuwanga saa moja jioni!! [emoji2][emoji2]
Huko unakuta msukuma ana ng’ombe 50-100 ila anakula ugali na dagaa wa mwanza wale gredi ya mwisho kabisa ambao huwa kwaajili ya vyakula vya Kuku!![emoji2][emoji2] huko ikifika saa 12 jioni tembo kutoka serengeti wanaingia kijiji kula miwa[emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Mwakaleli- Tukuyu Mbeya. Aisee baridi lilinishinda pale Mwax sec.
Acha uongo mwakaleli huduma za kijamii zote zipo baridi ikikushinda wewe siyo kigezo Cha kushindwa kuishi wengine
Unavyoonesha ukienda Ulaya Utakufa airport
 
Kijiji kingine ni mpyagula, kwa mbele kuna wasukuma wengi miaka ile wali na kambale mkubwa sana ilikua ni mia tano tu, mwenyeji wangu aliponiona kama nina mawazo akajadili na mke wake wakamwita binti mdogo wa mke wake aje anifariji chumbani na binti alikua mwanafunzi nilishangaa sana sitosahau hiko kisa
Tunda kimasihara[emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
[emoji16]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom