Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Tembea uone usingoje kuambiwa aliimba Dr Remmy Ongara

inaonekana hujatembea

Nenda Upareni kule juu Milimani
Kuna barabara ya lami hadi juu kabisa umeme upo wa uhakika,Maji ya bomba kabla ya uhuru yalikuwepo
 
Suji? Nilifika miaka 2 iliopita walikuwa wanamalizia kuweka lami ile barabara. Nilitamani kungekuwa kwetu.
 
Kuna sehemu moja huko Monduli nilifika umasaini yaani Kama hujakaza roho unaweza tafuta usafiri usiku kwa usiku.

Waweza jiona upo nyuma ya dunia maana Kila kitu ni shida, kuanzia umeme, maji, choo, nyumba ya kulala ni Kama tu kichuguu, dukani kufika kwa mguu ni lisaa na zaidi bado kurudi, hakuna hata kuangalia habari, jioni ni kuota Moto tu.

Ila wenyewe wamezoea na hawajali lolote.
Hapo shida labda iwe maji tu mengineyo yanazungumzika
 
Suji? Nilifika miaka 2 iliopita walikuwa wanamalizia kuweka lami ile barabara. Nilitamani kungekuwa kwetu.
Nenda Upareni sehemu inaitwa Usangi barabara ilikuwepo toka enzi ya Mjerumani na shule za seminari.Maji yapo toka miaka ya uhuru kule juu ni kijani kitupu watu wengi wanawachulia Wapare ni watu wa njaa sana wanaishi sehemu ya ukame wanasema hivyo wakichukulia kule tambarare Mwanga,Same,Kisangara na Hedaru ila ukweli ni kwamba ni kama mji wa Moshi ulivyo wapare wanakaa kule milimani kwenye maendeleo ya kutisha.
Kule huwezi kuta nyumba za majani hata siku moja kuna shule nyingi mno watu wa kule ni wasomi mno walimkubali mkoloni mapema mno na kupeleka watoto wao shule.

Nenda Suji nenda Mamba nenda Kihurio ndio utajua wapare ni kabila dogo lakini wana maendeleo makubwa mno Mshana Jr ni shahidi.

Aise karibu tena aisee mimi nimeoa huko nasifia ukweni
 
Kuna sehemu moja huko Monduli nilifika umasaini yaani Kama hujakaza roho unaweza tafuta usafiri usiku kwa usiku.

Waweza jiona upo nyuma ya dunia maana Kila kitu ni shida, kuanzia umeme, maji, choo, nyumba ya kulala ni Kama tu kichuguu, dukani kufika kwa mguu ni lisaa na zaidi bado kurudi, hakuna hata kuangalia habari, jioni ni kuota Moto tu.

Ila wenyewe wamezoea na hawajali lolote.
Kama wako na Dunia Yao hivii duuuu hatarrr
 
Nenda Upareni sehemu inaitwa Usangi barabara ilikuwepo toka enzi ya Mjerumani na shule za seminari.Maji yapo toka miaka ya uhuru kule juu ni kijani kitupu watu wengi wanawachulia Wapare ni watu wa njaa sana wanaishi sehemu ya ukame wanasema hivyo wakichukulia kule tambarare Mwanga,Same,Kisangara na Hedaru ila ukweli ni kwamba ni kama mji wa Moshi ulivyo wapare wanakaa kule milimani kwenye maendeleo ya kutisha.
Kule huwezi kuta nyumba za majani hata siku moja kuna shule nyingi mno watu wa kule ni wasomi mno walimkubali mkoloni mapema mno na kupeleka watoto wao shule.

Nenda Suji nenda Mamba nenda Kihurio ndio utajua wapare ni kabila dogo lakini wana maendeleo makubwa mno Mshana Jr ni shahidi.

Aise karibu tena aisee mimi nimeoa huko nasifia ukweni
Hongera mkuu
 
Zanzibar Michamvi... aisee km huwezi ishi ktk zile hotels au zile Bungalow za watalii ni shida, yaani wenyeji wanaishi ktk vinyumba vya makuti alafu kuona nyoka yupo ndani au kaning'inia juu ya mirunda ndani ni kawaida tuu 😅😅😅😅

Kwengine wilaya ya Tandahimba Mtwara, yaani kule ni msituni japo vijiji na watu wanaishi, yaani maji shida usafiri shida chakula ni Ming'oko na Panya kwa wingi, pombe no Bear kule ni Gongo (nipa) au Mnazi 😅😅😅 maji hata yakunawia uso asubihi ni deal.... sita rudi tena hizo pande kwakweli Duh!!
Ni kama Dunia nyiñgine hivi
 
Milo ipo Chalinze hapo karbu na ruvu unaingia kulia km20, kulikuwa na kambi ya wapigania uhuru wa South Africa miaka ya 80 adi 90 kwa sasa imegeuzwa kuwa zahanati ya kijiji.

Sio mbali sana ila barabara ni mbovu sana na mvua ikinyesha hakupitiki, kilichonishangaza kipind nafany mradi flani wa afya ni maisha ya kule kuna kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV, unaweza pima watu 10 ukakuta 6 wanao teyari au familia nzima wameathirika.
 
Kijiji kinaitwa Holo Iringa! Aiseee! Palivyokaa ni milima na mabonde yaani gari kuiona ni shida tofauti na Hiace moja ambayo ina ruti huko
 
Ismani kubwa sana ingawa kweli kijiji cha Ismani hakuna kituo cha mafuta na kwa Tanzania hii vijiji vingi havina vituo vya mafuta
Hadi Nyang'oro, kote hakuna vituo. Nimepazungumzia huko kwa sababu nililazimika kukaa hapo kwa wiki tatu kikazi, nami si shabiki wa videbe.

Kuna ukame balaa ila Watu wake wanakomaa kufuga kuliko kulima, wakiuhemea ule mto ambao kiangazi hali ni tete. Ila watu ni washkaji sana.

Ova
 
Back
Top Bottom