Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Tembea uone usingoje kuambiwa aliimba Dr Remmy Ongara

inaonekana hujatembea

Nenda Upareni kule juu Milimani
Kuna barabara ya lami hadi juu kabisa umeme upo wa uhakika,Maji ya bomba kabla ya uhuru yalikuwepo
 
Tembea uone usingoje kuambiwa aliimba Dr Remmy Ongara

inaonekana hujatembea

Nenda Upareni kule juu Milimani
Kuna barabara ya lami hadi juu kabisa umeme upo wa uhakika,Maji ya bomba kabla ya uhuru yalikuwepo
Suji? Nilifika miaka 2 iliopita walikuwa wanamalizia kuweka lami ile barabara. Nilitamani kungekuwa kwetu.
 
Hapo shida labda iwe maji tu mengineyo yanazungumzika
 
Suji? Nilifika miaka 2 iliopita walikuwa wanamalizia kuweka lami ile barabara. Nilitamani kungekuwa kwetu.
Nenda Upareni sehemu inaitwa Usangi barabara ilikuwepo toka enzi ya Mjerumani na shule za seminari.Maji yapo toka miaka ya uhuru kule juu ni kijani kitupu watu wengi wanawachulia Wapare ni watu wa njaa sana wanaishi sehemu ya ukame wanasema hivyo wakichukulia kule tambarare Mwanga,Same,Kisangara na Hedaru ila ukweli ni kwamba ni kama mji wa Moshi ulivyo wapare wanakaa kule milimani kwenye maendeleo ya kutisha.
Kule huwezi kuta nyumba za majani hata siku moja kuna shule nyingi mno watu wa kule ni wasomi mno walimkubali mkoloni mapema mno na kupeleka watoto wao shule.

Nenda Suji nenda Mamba nenda Kihurio ndio utajua wapare ni kabila dogo lakini wana maendeleo makubwa mno Mshana Jr ni shahidi.

Aise karibu tena aisee mimi nimeoa huko nasifia ukweni
 
Kama wako na Dunia Yao hivii duuuu hatarrr
 
Hongera mkuu
 
Ni kama Dunia nyiñgine hivi
 
Milo ipo Chalinze hapo karbu na ruvu unaingia kulia km20, kulikuwa na kambi ya wapigania uhuru wa South Africa miaka ya 80 adi 90 kwa sasa imegeuzwa kuwa zahanati ya kijiji.

Sio mbali sana ila barabara ni mbovu sana na mvua ikinyesha hakupitiki, kilichonishangaza kipind nafany mradi flani wa afya ni maisha ya kule kuna kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV, unaweza pima watu 10 ukakuta 6 wanao teyari au familia nzima wameathirika.
 
Kijiji kinaitwa Holo Iringa! Aiseee! Palivyokaa ni milima na mabonde yaani gari kuiona ni shida tofauti na Hiace moja ambayo ina ruti huko
 
Ismani kubwa sana ingawa kweli kijiji cha Ismani hakuna kituo cha mafuta na kwa Tanzania hii vijiji vingi havina vituo vya mafuta
Hadi Nyang'oro, kote hakuna vituo. Nimepazungumzia huko kwa sababu nililazimika kukaa hapo kwa wiki tatu kikazi, nami si shabiki wa videbe.

Kuna ukame balaa ila Watu wake wanakomaa kufuga kuliko kulima, wakiuhemea ule mto ambao kiangazi hali ni tete. Ila watu ni washkaji sana.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…