Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Tangeni bila shaka[emoji16] siku ya jumapili wanashuka milimani kuja kugonga kitimoto
Nilipanda mlima uluguru nikakuta waluguru huko juu Tena wanavijiji vyao Hali ya hewa ilikuwa nzuri ila huduma za kijamii Hadi uteremke mlima, binafsi nilishuka miguu inatetemeka na maumivu makali mno. Mpaka Leo nawashangaa watu Kule wanavyoishi
 
Nenda Morogoro shuka msamvu, chukua bodaboda akupeleke hadi shule ya msingi kikundi, nauli 1500.
Ukifika pale angalia mlimani kule watu wamejenga mlimani yaani. Sasa unajiuliza hawa watu hata mabati walipelekaje kule!
 
Mkuu uko ndiyo kwenye fursa ungewekeza kwenye ardhi
 
Tusilaumu Serikali kununua V8
 
Katikati ya mpanda na kigoma kuna pori wanauza chakula
 
Vijiji vya Vunta na Kidunda, Hedaru, wilaya ya Same.

Ni vijiji vilivyo milimani - ktk Safu ya milima ya Usambara.
Ukitokea Mombo, kabla ya kufika Hedaru, unakata kulia na kuanza songombingo la kupanda mlima kuelekea vijiji hivi.
Issue hapa ni barabara ya vumbi yenye slope kubwa ajabu! Dereva akifanya kosa kidogo tu, mmekwisha kwani gari litaserereka bondeni takribani mita 600 - 800 hadi litakapogonga mwamba na kusimama! Bila gari imara lenye 4-W, huwezi kwenda kule.
Wakati wa kurudi toka Vunta, nilimuuliza mwenyeji wangu kuwa kwanini hawa Wapare waliamua kwenda kuishi sehemu hatarishi kama zile? Aliniambia kuwa, Wapare walikimbilia kwenda kule kwa ajili ya maficho kutokana na vita kati yao na maadui zao pamoja na maasidi wao - Wachagga. Ilikuwa zamani sana kabla ya ujio wa Wakoloni.
Baadaye waliweka makazi mpaka leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…