Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,203
- 37,906
Mpwapwa ina vijiji vingi vya ajabu ajabu... kuna Kijiji kinaitwa MWENZERE .... hatari
Nzugilo Mpwapwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nzugilo Mpwapwa.
[emoji1][emoji1][emoji1]Hata tusiende mbali sana, wale raia wanaoishi ukingoni mwa bonge la mto Msimbazi ili tu waonekane wapo town...mvua zikianza wanahama nyumba, zikiisha wanarejea
🤣🤣🤣🤣UDOM-COED!
Kibwengo ndo niniKwa konje, handeni iko ndani ndani masaa sita kwa baisikeli kutoka makuyuni. Kila nyumba ina kibwengo
Nilipanda mlima uluguru nikakuta waluguru huko juu Tena wanavijiji vyao Hali ya hewa ilikuwa nzuri ila huduma za kijamii Hadi uteremke mlima, binafsi nilishuka miguu inatetemeka na maumivu makali mno. Mpaka Leo nawashangaa watu Kule wanavyoishi
Huwezi kuamini kuna watu wanaishi huko wewe unakoona hakuna makazi..wengi ni wafugaji! Tanzania ni kubwa sana..wanasema tembea uone!
Kilimanjaro so far sijaona maeneo yake yakitajwa.
Huko sidhan kama mazingira ya kuish ni magumu kiasi hicho kwan kiasi kikubwa huduma zote za kijamii zinapatikana
😂😂😂😂 halafu usiku saa tano, mimi huwa napatwa na mawazo sana, hawa wanaenda wapi?Vijiji vya njiani ukiwa unapita kwenda mikoani unakuta mtu anatembea kuelekea uelekeo ambao ww huoni nyumba
Mkuu uko ndiyo kwenye fursa ungewekeza kwenye ardhikijiji cha tanganyika,kata ya masagati tarafa mlimba wilaya ya kilombero .nikipangiwa kule kituo cha kazi mwaka 1999 nikarudi kumshukuru DED kwa kazi.nikarudi zang Dar .aise Kule watu alikuwa wanaishi kama mazombie hakuna huduma ylza jamii hata moja hadi uende mlimba 150km Dahhh ila nasikia mambo siku hizi yamebadilika Luna kula kitu japo afadhari.
🤣🤣🤣🤣UDOM-COED!
Tusilaumu Serikali kununua V8Kijiji cha Kitapi, kipo wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani. Kipindi nimehamishiwa kikazi nimekuta maji ni kuchota visima vifupi, barabara imefunikwa na manyasi, hakuna mtandao wa simu hadi upande kwenye miti, nyumba zipo mbalimbali na zipo msitu, huduma ya soko ni kuanzia saa kumi Jioni hadi saa kumi na mbili jioni mchana watu wapo shamba, giza linaanza saa kumi na moja jioni kwa sababu ya msitu mnene, hakuna bodaboda zaidi ya zinazokuja na kutoka, mvua ikinyesha hakuna safari tena sababu ya utelezi na matope, husikii muungurumo wa gari kwa sababu gari pekee ni wakati wa mitihani ya darasa la saba.
Katikati ya mpanda na kigoma kuna pori wanauza chakulaHabari za muda huu wanajf.
Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya
Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?
Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.
Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.
Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?