Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.

Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.

Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.

Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.
Watu wanachimba dhahabu ndani ya msitu wa amazon. Hakuna uhusiano wa madini na maji.
 
Tanganyika nako sio Mchezo? Kuna vijiji huko Tanganyika tukienda kupora ardhi yaani maarshi yapo ya kumwaga. Tuliendaga kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese kupora kujigawia ardhi miaka hiyo. Tuliingia kitongoji kimoja, Ng'ombe za wasukuma zikaja na kulizunguka Gari ilikuwa Land cruiser nyeupe na kuanza kuilamba. Tuliendaga Mishamo kwenye kambi za wakimbizi, ukipita Wamama wanakuja kuchukua ule mchanga ambapo tairi la gari limepita eti ni dawa kwa mtoto aliyechelewa kutembea.
Aisee kati ya visa vyote hiki ndio kimeniacha hoi.🤣🤣🤣
 
kuna mtu amewahi kufika kijiji kinaitwa “mbaa na vya mbele yake”? Ruvuma huko?2013 nilifika hakukuwa na mawasiliank yoyote ya simu ,ukihitaji mfanye mawasiliano hadi msogee kwenye baadhi ya miinuko mikubwa inayofahamika hivyo hapo utakuwa watu wengi kila mtu anafanya mawasiliano na usafiri gari zikifika kwenye milima mnashuka ipande yenyewe kwanza abiria ndio mfwate,gari ikipita wanaikimbilia na kuiimbia

Nilienjoy safari na mazingira ya beach sio mchanga ni mawe na fukwe zake unaweza kwenda umbali mrefu bila kuzama
 
Maeneo yale si shida kwa jeshi labda miundombinu ya barabara tu na makazi ya raia ,taliri ndio Inashare Geti na jkt si ndio kila chuo? Vianzi iko direction ipi kwenye ule mji?ni ndani ya eneo la jeshi? Sijaona jina hili Eneo la ramani
Nyuma huku kabla hujafika geti la jkt kuna majengo makubwa ya wajerumani huko ndy panaitwa vianze kwasasa majengo hayo yanatumiwa na taliri kama maboma ya mifugo tu
 
Vijiji vingi vya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu utashangaa wasukuma Sijui walifata nini huko, unakuta kijiji hakina umeme Wala maji. Yaan Maji yao wanachimba mabwawa kipindi cha mvua Maji yanatuama humo basi ng’ombe na binadam wote ndo mnakunywa Maji hayo!! Maji Kama maziwa kuna wachawi huko sijapata ona!! Wanga wananza kuwanga saa moja jioni!! [emoji2][emoji2]
Huko unakuta msukuma ana ng’ombe 50-100 ila anakula ugali na dagaa wa mwanza wale gredi ya mwisho kabisa ambao huwa kwaajili ya vyakula vya Kuku!![emoji2][emoji2] huko ikifika saa 12 jioni tembo kutoka serengeti wanaingia kijiji kula miwa[emoji23][emoji23]
Ukienda huko meatu itilima ndio hakufai kabisa unakutana na kuna Bushmen na mishale yao kwa bega [emoji1787]
 
Hahaaaa, ni nimetoka huko toka 2014. Huko sio mchezo jamaa nasikia walikuwa wawindaji ndio maana waliishi huko. Niliendaga huko kuwinda Wanyamapori na kuchana mbao za Miminga na Mikora. Operation tokomeza ilinipitia ndio nikakimbia. Maisha haya
Haaa haaa Pole mzee, nilikuwa huko last week nazunguka na mwenge, Nchi hii ina maeneo ukifika unaishia kupigwa butwaa
 
Habari za muda huu wanajf.

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?
Ukara island lake Victoria
 
Back
Top Bottom