Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ilunde Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi. Kijiji kipo Porini, Kilomita 70 toka makao makuu ya Wilaya ya Mlele. Hakuna network wala nini na ni Porini hasa. Sijui walifuata nini kule.
Mkuu, ulienda kufanya nini huko
Nipo Mpanda mjini ila naona jau, Sasa ingekua nipo huko Sijui ingekuaje
 
Umeandika pumba mdau.

Kwamba maendeleo ya nchi yanaenda na ukubwa wa eneo?

Kwamba ENGLAND inazidiwa maendeleo na Tanzania kwa kuwa ina eneo dogo?
Yah ni kweli ata Zanzibar kuna maendeleo kushinda Tanganyika, Nimeishi Zanzibar sikuwahi kuona Wamama wakipata shida ya maji na huduma za hospitali na usafiri, umeme upo kila sehemu, sehemu zote za Tanzania Zanzibar hawana shida za huduma za kijamii huduma zote zimewafikia wananchi, tembea Zanzibar kote huwezi kukuta mama kabeba ndoo ya maji kichwani , na uko vijiji huduma zote zipo, yani Zanzibar kuna vitu vingi vya elektroniki mpaki vijijini, Zanzibar mtu kukupa nyumba uishi au kukuazima gari lake uendeshe ni jambo la kawaida tena uko ni mashambani.
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.
Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.View attachment 2378247
Na wakati wanajenga huko,usagara kulikuwa na viwanja vya bei nzur,huwa najiuliza wakiwa wanamatatizo ya kiafya wanapandaje maana mwili unahitaji utumie nguvu nyingi hata wakat wa kushuka inatakiwa utumie nguvu za kujibalance usiseleleke sana
 
Mkuu, ulienda kufanya nini huko
Nipo Mpanda mjini ila naona jau, Sasa ingekua nipo huko Sijui ingekuaje
Maisha haya Mkuu, nilikuwa nawinda wanyamapori na kupasua mbao za mininga na Mikora huko. Operation tokomeza majangili ndio ilinikimbiza huko. Hivi yule Kombe alikuwaga na Duka la Dawa baridi yupo na duka lake lipo? Huko Ilunde sio mchezo miaka hiyo, kunasa kwenye mchanga ilikuwa ni kitu cha kawaida. Kuna kipindi tukikosa maji Porini ikabidi tuvue mashati yetu tulipofika sehemu kilipokuwa na tope, tukaweka tope na kuanza kulikamua via mashati yetu ili tupate maji. Salimia sana Zozzi Family, Kafirika, Mallack Family, Dotto Njeni hapo Mpanda.
 
Yes, Rukwa Kuna madini sana
Huyo hapajui Majimoto na sio pabaya ni sehemu nzuri na muda si mrefu panaweza kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo. Pale ni pazuri sana na pana Mzunguko mkubwa sana wa Biashara hususan za Mpunga, Ufuta n.k pale kulikuwa na matajiri sana akina Madirisha kipindi hicho. Sasa panaonekana patakuwa pamefunguka sana kwani Kuna barabara ya lami na lile daraja la Kavuu la kutokea Inyonga limeisha na linatumika. Kulikuwa na kitongoji kimoja kinaitwa Centre kichaa kule maji moto kwa ndani. Aiseeee, kule unamkuta msukuma mwanaume kavaa sketi ya shule na kanga huku amesuka nywele na kuvaa heleni kama mwanamke. Kule jamaa wanavuta bangi tu, kwanza nyumba zao zilikuwa ni za Masuke ya Ufuta.
 
Ukerewe kisiwa Cha Irugwa huko watu hawana vyoo wanajisaidia vichakani na kwenye miamba wanawake na wanaume wanaoga pamoja ziwani unakuta wako wengi utazani mnada nikaenda maeneo ya Musoma Kwa wajita nikakuta Hali Iko hivyo sema wao Wana vyoo ila Bado wanaoga pamoja
 
Hivi ilikuwaje makete yakawa makazi ya binadamu! Huwa najiuliza mbona nchi yetu ina eneo kubwa sana la ardhi watu walivutiwa na nini huko makete? Kuishi makete ni adhabu, narudia tena kuishi makete ni adhabu.
 
24/7 watu wamelewa tu huko,kinachowalewesha Ni harufu ya mavi Muda wote.
mabibo pale mwisho kuna kama bwawa hivi ,mshenzi mmoja ana kiwanda cha nguo maeneo yale anatiririsha maji ya kemikali ndani mle yanakaa e banaa eeeh yakioza yakavunda yale harufu yake nya na ndugu yake ushuzi wakasome tena chuo chao kikuu cha kutoa harufu.
 
Back
Top Bottom