Ni sikio la kufa? Mama anaitupa kadi yake muhimu ya kukubalika kwake

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
Salamu mbele!

Walio wengi huku mtaani wanaona hafai kuvaa si tu viatu bali hata soksi za mwendazake, sifa pekee inayomtofautisha na mtangulizi wake ni hii Sifa ya demokrasia na utawala bora.

Hivi karibuni ameonekana anaitupa hata hii karata muhimu inayomtofautisha na mtangulizi wake ambayo angalau inafanya watu waliokuwa hawamkubali mtangulizi wake tumuone yeye ana nafuu kidogo. Sifa iliyofanya akubalike si tu Tanzania hata na wafadhili huko nje, ajipatie mikopo na misaada kedekede.

Hii kamata kamata ya wakosoaji itamfanya afananishwe na mwendazake na akifika hapo si viatu wala soksi zinamtosha.
 
Na Bado mtanyooshwa Hadi muongee yote mlikuwa mnaleta dharau na kutumia vibaya uhuru Mliyopewa.
Wewe ni mjinga. Hakuna atakayenyoshwa na huyu mama. Uwezekano mkubwa atapindishwa yeye hadi avunjike.

Mnamjaza ujinga ili aharibikiwe. Ana uamuzi wa kuchagua, afuate ushauri wa kijinga toka kwa wajinga au ushauri wenye manufaa toka werevu.
 
Salamu mbele!

Walio wengi huku mtaani wanaona hafai kuvaa si tu viatu bali hata soksi za mwendazake, Sifa pekee inayomtofautisha na mtangulizi wake ni hii Sifa ya demokrasia na utawala bora.

Hivi karibuni ameonekana anaitupa hata hii karata muhimu inayomtofautisha na mtangulizi wake ambayo angalau inafanya watu waliokuwa hawamkubali mtangulizi wake tumuone yeye ana nafuu kidogo. Sifa iliyofanya akubalike si tu Tanzania hata na wafadhili huko nje, ajipatie mikopo na misaada kedekede.

Hii kamata kamata ya wakosoaji itamfanya afananishwe na mwendazake na akifika hapo si viatu wala soksi zinamtosha.
Huyu mpaka hapa alipo, hakuna kiongozi anayeweza kumfikia kwa uovu. Hakuna mtawala yeyote alitewahi kuwabambikia wakosoaji wake kesi za uhaini.

Kesi ya uhaini hukumu yake ni kifo. Ina maana, huyu ameingiwa na hamu ya kuwaua wanaomkosoa, japo hatafanikiwa. Lakini ameonesha nia hiyo.
 
Wewe ni mjinga. Hakuna atakayenyoshwa na huyu mama. Uwezekano mkubwa atapindishwa yeye hadi avunjike.

Mnamjaza ujinga ili aharibikiwe. Ana uamuzi wa kuchagua, afuate ushauri wa kijinga toka kwa wajinga au ushauri wenye manufaa toka werevu.
Wangapi wako kolokoloni wananyooshwa? Na wewe kaongee uhaini uone moto ndio tutajua wewe au yeye nani mjinga
 
Halafu mwisho wa haya yote, mtapata nini? Walikuwepo akina Adolf Hitler, Benito Musolini, Iddi Amin Dada, na wengineo wengi! Leo hii wako wapi?
Nchi itakuwa na amani mstarehe saaaafi kabisa.

Kwani nyie mlikuwa mnaleta taharuki Ili mkikinukisha mkimbilie Kwa mabwana zenu Ulaya si ndio? Mtavunjika nyie kabla yetu.
 
Salamu mbele!

Walio wengi huku mtaani wanaona hafai kuvaa si tu viatu bali hata soksi za mwendazake, sifa pekee inayomtofautisha na mtangulizi wake ni hii Sifa ya demokrasia na utawala bora.

Hivi karibuni ameonekana anaitupa hata hii karata muhimu inayomtofautisha na mtangulizi wake ambayo angalau inafanya watu waliokuwa hawamkubali mtangulizi wake tumuone yeye ana nafuu kidogo. Sifa iliyofanya akubalike si tu Tanzania hata na wafadhili huko nje, ajipatie mikopo na misaada kedekede.

Hii kamata kamata ya wakosoaji itamfanya afananishwe na mwendazake na akifika hapo si viatu wala soksi zinamtosha.
Hivi hizi shahada za heshima za udaktari ambazo baadhi ya watu wasiostahili wametunukiwa kimakosa ama kwa kupitia "undue influence or duress" kuna utaratibu wa kuweza kuzifuta?

Endapo muhusika haonyeshi kabisa dalili ya kukidhi sifa ya kustahili tuzo husika, mchakato wa ku "refute" ama ku "revoke" unawezekana? Naona shahada za namna hii ndizo zenye kusababisha baadhi ya viongozi kubweteka na kupoteza uelekeo kabisa.
 
Wangapi wako kolokoloni wananyooshwa? Na wewe kaongee uhaini uone moto ndio tutajua wewe au yeye nani mjinga
"kuongea uhaini" ndiyo nini? Weka mifano. Uhaini unafanywa au "unaongelewa" waziwazi in public majukwaani?
 
Wamezunguka nchi nzima kujaribu kupotosha (ingawa wao walidai wanaelimisha) juu ya kuuzwa kwa bandari. Wameona wananchi hawawaelewi yaani wananchi wamewaelewa akina Mwabukusi kuliko akina Bibi na akina mr. MWONGO. Baada ya kushindwa hoja sasa wanajaribu kuwatesa. Kuwafunga na kuwafungulia kesi za uhaini. Kwanza neno lenyewe UHAINI ni gumu mno. Aliyesema anawaunganisha Watanganyika sasa anajaribu kuwabomoa kwa kasi sana. Lakini hataweza maana mara nyingi watu huungana yanapotokea matatizo.
 
Back
Top Bottom