Ni starehe ipi ambayo huwezi kuiacha, hata kama ushauriwe kiasi gani?

Ni starehe ipi ambayo huwezi kuiacha, hata kama ushauriwe kiasi gani?

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
31,913
Reaction score
65,514
Salaam wakuu, unajua katika maisha haya. Kuna baadhi yetu tumekuwa tukifanya baadhi ya vitu ambapo vimekuwa vikitufurahisha.
kiasi kwamba imekuwa ngumu kuacha, hata Kama tushauriwe kwa ukubwa gani, au na mtu yoyote.

kwa upande wangu Kuna vitu vinne, naona kabisa kuacha ni mpaka niingie kaburuni.

👉Misosi- najua mtasema kila mtu anakula, ila kwa upande wangu bhana naona imezidi.
Maana nimeshaifanya kesi, kila nikikutana nacho ni mpaka mmoja wetu anyooshe mikono juu (hapa adui yangu nimemzidi aisee) napakia kiukweli, iwe ugali,wali,ndizi na hata iwe kachumbari
FB_IMG_16720535044134322.jpg

FB_IMG_16735545715844809.jpg


Kucheza magame, wakati nakua hili swala lilinafanya nitandikwe Sana na wazazi.
Kwani ilikua huniambii kitu linapokuja swala la kucheza game-nimetumia gameboy, PlayStation.
Mpaka leo imepelekea kuwa Kama moja ya mila na tamaduni zangu, siwezi kukaa bila kucheza magame iwe kwenye pc, PlayStation na hata kwenye simu.
Nimecheza game Kama 👉 asphalt series zote.
👉Pes hadi ya mwaka huu.
👉 Brother in arms 2&3
👉Call of duty.
👉Motorcombat iwe la porin au jeshi.
👉Fifa

Kusoma vitabu, huu ni mmoja ya utaratibu wangu unaonivutia sana.
I didn't have a great childhood life. hivyo niliamua kufunga ndoa na vitabu, nimesoma vingi Sana,ambavyo vilinisaidia kujifunza na kuelimika Sana.
Baadhi ya vitabu nilivyosoma katika Safari yangu hii👉magic of thinking big
👉The 5am club
👉The godfather
👉 Retire young, retire rich.
👉The billionaire of tommorow.
👉What the future.
👉Alex rider
👉 Intelligent investor.
👉Elon musk
👉 Business in Africa.
Hiyo ni list ya baadhi tu, so unaeza tafuta ukajifunza na kufurahia pia.

Kutazama movie,series na documentary, Mimi ni jobless wa kimataifa.
hii imekuwa fursa kubwa kwangu, kwani imenipa nafasi ya kufatilia series na movie nyingi sana.
ziwe crime,horror,drama, investigation, na hata animation. List ya series nilizotazama👉money haseist
👉24 hours.
👉Prison break
👉 Vikings
👉Dracula
👉Jumong
👉Iris
👉 Harry Potter
👉Lord of the rings.(smigo)

Acha niendelee kufurahia uwepo wangu duniani.

wametokea washauri wengi "eti punguza", ninachowajibu ni kwamba wao ni wageni kwenye maisha yangu hivyo wanaeza kwenda..

Ni vitu gani imekuwa ngumu kwako kutengana navyo??
 
Back
Top Bottom