Lucas philipo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2017
- 2,039
- 2,676
Umeeleza kwa kina!!Uelewa gani ambao hana Mch. Gwajima ambao wewe unao G Sam..?
Hata hivyo:
1. Mwenzio anazungumza mambo katika perspective ya kiroho, ambayo wewe naamini kuwa huna uelewa huo...
2. Hata katika perspective ya kisayansi anaelewa kuliko unavyoelewa wewe. Mfano hoja za kisayansi za Mch. Gwajima ni;
#1. Hakuna utafiti wa kutosha wa kisayansi uliokwisha kufanyika kuthibitisha usalama wa chanjo yeyote ya korona mpaka sasa. Kama upo weka paper yake hapa uoneshe ilichapwa lini, wapi na nani. Kama hakuna, haraka ya nini kutaka kulazimisha kila mtu achanjwe pasipo kuwa na scientific safety assurance kwanza..?
#2. Nini madhara ya chanjo hii ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwa atakayechanjwa..?
#3. Kwa maneno ya Rais Samia Mwenyewe siku ya uzinduzi wa chanjo kitaifa alisema kuwa, mara mtu achanjwapo anaingia moja kwa moja kwenye database ya dunia. Swali, ni nani mmiliki wa database hiyo? Yuko wapi?
Haya ndo maswali anayouliza Mch. Gwajima na watetezi wa hii kitu wanakwepa au wanashindwa kutoa majibu sahihi...!!
Kama mtu makini hajiulizi maswali haya kabla ya kupokea hii kitu, basi huyo mtu ndiye mjinga kabisa kwa 100%...!!!!
Wala huibiwi ardhi kwa njia na namna hiyo ujuayo wewe. Aidha ili kujibu hoja hii, ni lazima kwanza ujibu swali la #3 hapo juu...
Hata hivyo, si kweli kuwa, huko walikotengeneza chanjo hizi wote wanachanjwa. Wapo tena kwa maelfu wenye misimamo kama ya Mch. Gwajima hapa Tanzania...!!
Absolutely, Mungu wetu ni wa kipekee. Anatupenda sana. Sijui ni kwanini wewe huuoni upendo huo...!
Imeandikwa;
"...hamkosi kuzitambua hila (mikakati) yake (yaani ibilisi/shetani)...."
Si kila kilicho kizuri kwa kuonekana kwa sauti au kwa dhamira chatoka kwa Mungu. Mwombe Mungu akupe uwezo wa kuzitambua hila zake mbaya za uangamivu...!!
Hata hivyo, kuchanjwa ni hiari. Tumia uhiari wako kuamua kwa busara na kwa usalama wako. Kwa hili, chagua Mungu katika Yesu Kristo. Kwake ni guaranteed usalama kwa 100%....!!
Shida mihemko, wanashindwa kujibu hoja za msingi za Gwajima!!