Kuna taarifa nyingi ziliniacha na furaha kubwa kwani mengi sikuwahi hata kumuomba Mungu wala kuwazia kuwa nastahili.
Moja nilipofaulu form 6, nikiwa private candidate baada ya kushindwa kwenda shule kwa kukosa ada na nauli tu. Nikajiunga UDSM, nikapata shida kubwa(sitaki hata kukumbuka), hata sijui ilikuwaje nikamaliza Chuo, ukiniuliza siwezi hata kukumbuka ilikuwaje nikamaliza Chuo.
Ajabu la pili hata niliite ajabu, kabla ya wiki 1 kwa UE mwaka wa mwisho nikampoteza Mama yangu kipenzi, huyu ndio tumaini langu pekee lililokuwa limebaki ukiachia Mungu. Ilikuwa ngumu kurudi kufanya UE, ila nikarudi Chuo nikaingia kwenye paper nikijua nakamilisha idadi tu ya wanaotarajia kumaliza Chuo ila sitoboi.
Baada ya paper, nikarejea kijijin kwetu ili nikajipange kwenda kuripoti Ukerewe ambako nilipangiwa kwenda kama Mwalimu...Kwa wale wa 2009 wanajua tulikuwa tukipangiwa vituo hata kabla ya matokeo ya mwisho kama sikosei. Kabla sijaondoka nikapigiwa simu na rafiki yangu akaniambia kuna shirika wanatafuta Walimu, nikataka kumpotezea kwani nilijua hata GPA yangu haitakuwa kivutio. Ila jamaa alinisihi mno, kwani anajua uwezo wangu pamoja na muda mwingi kutoutumia darasani ila kwenye presentation aliona kitu kwangu.
Baada ya kufika Dar tu nikaulizwa nina passport ya kusafiria? Nikashangaa, nikapewa mtu pale uhamiaji akanifanyia utaratibu nikapata passport kesho yake nikaikabidhi kwa mhusika. Bila kuambiwa kitu, nikapelekwa Mikocheni nikawakuta wenzangu 7 tukawa 8.
Taarifa ikawa tunasafiri week ijayo kwenda nje kwa wiki 2 kujifunza mambo(nchi nitaihifadhi). Hapo niliamini Mungu ni mwenye huruma sana.
Nilirudi nikapewa ajira kwakweli sikuwahi kuamini kama nilistahili, ila ninachokiamini nilikuwa na uwezo mkubwa mazingira tu ndio yalikuwa magumu. Niliitendea haki kazi niliyopewa.
Nilizunguka Duniani mpaka mwaka 2016 hapo ndio nilipata jaribu la maisha tena, nikiwa safarini nilipata ajali mbaya iliyopelekea mauti ya Mama wawili niliowapa lifti tu(RIP Wamama ), Nikapoteza matumaini tena, sikiweza kwenda kazini tena, pamoja na kupewa muda ila nilikuwa kama mtu aliyerukwa na akili.
Mwaka 2017 nikajaribu kuomba program fulani US, siku nilipopata Email na simu ya kuwa shortlisted nikakumbuka Mungu ananipenda mno kwani niliamini labda sina sifa na watu niliokutana nao kwenye interview niliamini wananizidi kuanzia matokeo ya darasani, Nikafanikiwa na kuwa finalist, ila ikawa nifanye TOEFL then tusubirie zaid ya miezi 5 mbele kujua nani na nani wataenda.
Nikaanza kula msoto, nikapoteza hata marafiki na ndugu mbona ukisikia kufulia ndio huko. Hili jambo sikumuambia mtu yoyote yule zaidi, kwahiyo aliyekuwa anajua ni wale finalist wenzangu tu ambao tumejuana tulipofikia hatua hiyo. So hakuna mtu anajua nasubiria bahat ya kutimkia US.
Ilipofika mwezi wa 9, natoka zangu kuswali, ile kuwasha simu nakutana na Email ilibidi niswali Sunna kwanza labda sijaona vizur, hatimae mimi ni miongoni mwa wanaoenda US...
Nini nataka kusema?? Kila gumu lina suluhisho mbele ya Mungu, katika taarifa nzuri nilizowahi kupokea, 90%sijawahi kutegemea wala kumuomba Mungu.