Ni tetesi gani zilivuma sana miaka ya nyuma lakini hazikuwa za kweli?

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
11,452
Reaction score
10,059
Ni tetesi au habari zipi unazokumbuka ambazo zilivuma sana enzi hizo lakini hazikutokea.

Ninazozikumbuka ni pamoja na tetesi kamba dunia ingefika mwisho mwaka 2000. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanaamini kabisa lakini haikutokea

Kuna waliouza nyumba, mashamba, na magari yao kwa bei ya chini sana. Walifanya hivyo wakiamini kuwa baada ya mwaka 2000 mali hizo hazitakuwa na thamani tena.

Baadaye mwaka 2000 ulipoingia salama, wengi walipata mshtuko wa kiuchumi na kulazimika kununua tena mali zao kwa bei ya juu sana.

Lakini pia kwenye miaka ya 1970, 1980 hadi mapema 1990 kulikuwa na imani iliyoenea sana kuwa kuna kikundi cha watu (mara nyingi walihusishwa na matajiri wenye magari meusi ya kifahari au watu weupe) wanaoteka watu usiku na kuwanyonya damu yote kwa kutumia sindano kubwa au mashine maalum kwa ajili ya mambo ya kishirikina au biashara.

Pia kuna stori za chuma ulete na nyinginezo kama hizo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
kulikua na mnyonya damu tishio anaitwa Msekwa, walikuwa wanasema eti anamiliki Peugot 504 nyekundu na haina mlio kabisa...basi tulikuwa hatutembei nje zaidi ya saa 12 jioni....
 
Wanyonya damu tukiona land cruiser tuna toka ndukii..

Enzii za wachuna ngozii MBOZI MBEYAA

Wapiga nondo ili wauze mabucha.. MBEYA
 
Story za Nguva, popobawa, uviumi wa wazee wa 'kimila' ndani ya maji ilipozama Mv Bukoba kusema 'miili iliyoopolewa imetosha'
 
kulikua na mnyonya damu tishio anaitwa Msekwa, walikuwa wanasema eti anamiliki Peugot 504 nyekundu na haina mlio kabisa...basi tulikuwa hatutembei nje zaidi ya saa 12 jioni....
Tena walidai alikuwa ana titi moja,tombo dimwe😊😊😊
 
Mi naona mambo ya wakati ule yalikuwa mazuri kuliko ata ya Sasa hivi 🤔
 
Ni tetesi au habari zipi unazokumbuka ambazo zilivuma sana enzi hizo lakini hazikutokea.

Ninazozikumbuka ni pamoja na tetesi kamba dunia ingefika mwisho mwaka 2000. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanaamini kabisa lakini haikutokea

Kuna waliouza nyumba, mashamba, na magari yao kwa bei ya chini sana. Walifanya hivyo wakiamini kuwa baada ya mwaka 2000 mali hizo hazitakuwa na thamani tena.

Baadaye mwaka 2000 ulipoingia salama, wengi walipata mshtuko wa kiuchumi na kulazimika kununua tena mali zao kwa bei ya juu sana.

Lakini pia kwenye miaka ya 1970, 1980 hadi mapema 1990 kulikuwa na imani iliyoenea sana kuwa kuna kikundi cha watu (mara nyingi walihusishwa na matajiri wenye magari meusi ya kifahari au watu weupe) wanaoteka watu usiku na kuwanyonya damu yote kwa kutumia sindano kubwa au mashine maalum kwa ajili ya mambo ya kishirikina au biashara.

Pia kuna stori za chuma ulete na nyinginezo kama hizo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mwaka 2000 kungetokea vita kubwa sana dunia nzima, na huo ndo utakuwa mwisho wa maisha ya duniani
 
Mitaa niliyoishi enzi hizo kulikuwa na stori ya vibwengo, kwamba ukipita usiku kuanzia saa 2 usipowasalimia utakoma. Wana wewe watakupiga hawakuachi.
Na pia vifuu vinavyocheza ngoma unaweza kukutana navyo usiku
 
Back
Top Bottom