Ni tetesi gani zilivuma sana miaka ya nyuma lakini hazikuwa za kweli?

Ni tetesi gani zilivuma sana miaka ya nyuma lakini hazikuwa za kweli?

Ni tetesi au habari zipi unazokumbuka ambazo zilivuma sana enzi hizo lakini hazikutokea.

Ninazozikumbuka ni pamoja na tetesi kamba dunia ingefika mwisho mwaka 2000. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanaamini kabisa lakini haikutokea

Kuna waliouza nyumba, mashamba, na magari yao kwa bei ya chini sana. Walifanya hivyo wakiamini kuwa baada ya mwaka 2000 mali hizo hazitakuwa na thamani tena.

Baadaye mwaka 2000 ulipoingia salama, wengi walipata mshtuko wa kiuchumi na kulazimika kununua tena mali zao kwa bei ya juu sana.

Lakini pia kwenye miaka ya 1970, 1980 hadi mapema 1990 kulikuwa na imani iliyoenea sana kuwa kuna kikundi cha watu (mara nyingi walihusishwa na matajiri wenye magari meusi ya kifahari au watu weupe) wanaoteka watu usiku na kuwanyonya damu yote kwa kutumia sindano kubwa au mashine maalum kwa ajili ya mambo ya kishirikina au biashara.

Pia kuna stori za chuma ulete na nyinginezo kama hizo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Watu wazima hawajambi, sasa ndo tumekua watu wazima wenyewe.
 
Mambo mengine yalitokea isipokuwa mwisho wa dunia (2000)
 
Habari za popobawa, habari za wanyonya damu na habari ha Chunusi huko baharini, labda Mshana Jr atakuja kutoa ufafanjzi mzee wa vilingeni...
 
Back
Top Bottom