Story yangu ni kama movie
Kuna bint alikua kanitangulia darasa 1. Yeye alikua la pili mimi la kwanza. Huyu bint tulifahamiana mtaani tukiwa majirani baadaye sisi tukahamia kota za shule coz mzee alikua teacher. Alikuwa na binam yake nasoma naye la kwanza. Akampa kibarua cha mapenzi kimeandikwa kwa penseli na muandiko una makosa makosa mengi tu aniletee. Nafikiri huyu binam ndo alishawishi kipenzi changu aandike kibarua kile maana yeye alikua machepele kidogo.
Yule bidada akaja kunipa kile kikaratasi darasani. Kuna njemba 2 tulikua tunasoma nazo zilikua kubwa sana zikaona ile issue. Wakawa wanakomaa niwape ile karatasi wasome. Mimi sikuwapa. Mara ghafla mwalimu akaingia akakuta mzozo. Alipouliza njemba moja ikasema....huyu Meraki ana karatasi yangu hataki kunipa. Mwalimu akasema nimpe nikadai mimi sina. Jamaa likakomaa kuwa ninacho mfukoni. Teacher mama yule akasema njooni huku mbele.
Tulipofika mbele mwalimu akanipiga sachi mfukoni na kutoka na kile kibarua. Akakisoma.....alipokisoma akabaki ameduwaa na akamuuliza njemba. Karatasi hii yako wewe au ya huyu Meraki? Jamaa kuona msala akasema sio yake ni yangu ila naye alitaka kusoma.
Mwalimu akanichukua akanipeleka ofisi ya walimu akaitwa na yule bint tukaanza kuhojiwa. Bint hasemi kitu wala mimi sisemi kitu. Tulikula stick sana. Stick zilipozidi nikakimbilia nje ambako kulikua na mvua. Waalimu wakawa wanashindwa kunifata. Nikasepa home. Ambako kulikua ni hapo hapo tu jirani.
Kufika home mama ananiuliza mbona umelowa mvua na unalia nini? Nikampiga fix nikachill home. Mfuko wangu wa madaftari aliniletea mtoto wa mwalimu mkuu ambaye alikua rafiki yangu sana wote tukiwa watoto wa kota. Uzuri siku hiyo baba hakuwa kazini so nikajua msala umeisha.
Kumbe msala ule maticha wamemwambia mama na kile kibarua wamempa mama aje kumuonesha dingi. Nilikuja kugundua hili baada ya kuja kuona ile barua juu ya kabati ambapo nilikuwa naweka mastafeli yaive.....nilipoweka stuli kupanda ndo nikaiona. Nikaichukua na kwenda kuichana nje kwenye mauwa.
Next morning bi mkubwa akiwa anafagia uwanja akaona vipande vya kile kikaratasi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Niliporudi shule mama akanisema kuwa nimeiba ile karatasi na kuichana nisubiri bakora za dingi. Ujinga wako unaoufanya huko shuleni nimeambiwa wote. Sasa umsubiri baba yako.
Mpaka leo sijaju kama mama alimwambia baba.[emoji28]
Ngoja siku nikienda kwa mama nimkumbushe hii story....na yule bint Farida ambaye hata yeye alikua akimpenda sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app