Ni tukio gani lilitokea ukiwa mbali na mazingira husika ukatamani ungekuwepo kwa muda huo?

Kama una watoto ndani, umakini unahitajika sana, hasa chumba chao wanacho lala,
 
Vifo na magonjwa ni matukio ambayo huwa kama binadamu yakitokea huwa tunatamani laiti tungekuwapo huenda tungebadili matokeo. Ila ndio ufundi wa mwenyezi Mungu kutufumba yajayo.
Kweli mkuu, haya mambo hayazuiliki kutokea. Kwa upeo wetu wa kibinadamu kuna muda tunaona tunaweza zuia lakini sio haiwezekani.
 
Kweli mkuu, haya mambo hayazuiliki kutokea. Kwa upeo wetu wa kibinadamu kuna muda tunaona tunaweza zuia lakini sio haiwezekani.
Rafiki yangu alipata ajali ya gari. Akawaambiwa waliomukoa watizame simu yake wampigie simu mkewe na mimi. Mkewe nae akanijulisha kuwa ameongea na jamaa anasisitiza twende hospitali. Tulienda ingawa kwa kuchelewa kama saa moja. Sikufanikiwa kuongea. Na siku hiyo hiyo alifariki dunia. Maumivu aliyoniachia sijawahi yafananisha na chochote. Hua natamani laiti ningewahi hospitali siku hiyo utafikiri kuna vitu vya ziada ningeweza fanya kugeuza matokeo. Sababu huduma alipata. Ila ndio hivo aliumia viuongo vya ndani.
 
Pole sana bro
 
Personally, sijawahi jutia chochote pia nimeiambia nafsi yangu kutojutia chochote ni kuchosha moyo na akili

Live in the moment, cherish the past embrace the future 🙏
 
Personally, sijawahi jutia chochote pia nimeiambia nafsi yangu kutojutia chochote ni kuchosha moyo na akili

Live in the moment, cherish the past embrace the future 🙏
That you havent come across any situation that you havent never wished it would have gone down the other way around? Looks like you are in plain denial if you a mortal just like the rest of us.
 
Pole sana inauma nilipoteza rafiki pia
 
Pole sana mkuu huenda alikuwa na maelekezo muhimu sana alitaka akushirikishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…