Rafiki yangu alipata ajali ya gari. Akawaambiwa waliomukoa watizame simu yake wampigie simu mkewe na mimi. Mkewe nae akanijulisha kuwa ameongea na jamaa anasisitiza twende hospitali. Tulienda ingawa kwa kuchelewa kama saa moja. Sikufanikiwa kuongea. Na siku hiyo hiyo alifariki dunia. Maumivu aliyoniachia sijawahi yafananisha na chochote. Hua natamani laiti ningewahi hospitali siku hiyo utafikiri kuna vitu vya ziada ningeweza fanya kugeuza matokeo. Sababu huduma alipata. Ila ndio hivo aliumia viuongo vya ndani.